farmented grape afu Haina kileo? Kabla ya hapo lutu alikua anakunywa au ndo ilikua siku yake ya kwanza???
Divai aliyotengeneza Yesu haikuwa fermented. Lakini ile aliyokunywa Lutu ni wazi ilikuwa fermented.
Hata hivyo Biblia haionyeshi popote kwamba Lutu alikuwa anapenda ulevi kabla ya tukio hilo. Hakuna andiko linalosema alikuwa na tabia ya kunywa kila siku.
Tukio la Mwanzo 19 lilikuwa la kipekee – binti zake walimpa divai inayolevya kwa makusudi ili kumfanya apoteze fahamu na kutekeleza mpango wao wa dhambi.
Mwanzo 19:33 – "Basi wakamnywesha baba yao divai usiku ule..."
Mwanzo 19:35 – "Wakamnywesha baba yao divai usiku ule tena..."
Hii haionyeshi kwamba Lutu alikuwa mlevi wa muda mrefu, bali alinyweshwa pombe kwa hila. Kama angekuwa mlevi sugu, asingehitaji kunyweshwa kwa hila.
Kama ulevi usingekuwa mbaya, kwa nini tukio la Lutu lilikuwa na matokeo mabaya? Lutu alipokunywa:
-Alipoteza fahamu kabisa
-Alilala na binti zake bila kujua
-Alizalisha kizazi kilichokuwa maadui wa Israeli (Moabu na Amoni)
Hayo yote yanaonyesha moja kwa moja madhara ya ulevi. Lutu alikunywa na akafanya dhambi kubwa bila kujua, jambo ambalo linaendana na onyo la Biblia kuhusu ulevi:
Mithali 23:31-33
Usiutazame mvinyo iwapo ni mwekundu;
uitiapo bilauri rangi yake, ushukapo taratibu;
Mwisho wake huuma kama nyoka;
Huchoma kama fira.
Macho yako yataona mambo mageni;
Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;
Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
Utasema, Wamenichapa wala sikuumia;
Wamenipiga wala sina habari...