Hivi kuna maisha baada ya kifo?

Unafaa kuwa mwanasiasa brother.
Wanasiasa wana sifa ya kutojibu maswali, kwa sifa hiyo, wewe umenizidi mimi uanasiasa.

Nimekuuliza swali hata hujakubali kwamba umeliona.

Nakuuliza tena.

Nikikuuliza uchawi ni nini na unajuaje huu lazima ni uchawi, si kitu kingine chochote usichokijua, utajibu vipi?
 
So paka yule akitembea pale bila roho kafa au...mbona anaishi bila roho afu wewe ambae pia unaishi una roho?
Mimi pia ni kiumbe hai kama yule paka anayetembea pale.ila nina cha ziada ambacho ni roho.
Sijasema nataka niione roho nimekuambia ujibu hoja zangu na unipe verifiable evidence ya roho... sijawahi ona white blood cells ila naamini wapo coz Kuna non conflicting evidence.
Oops! Verifiable evidence ya roho kwa maana ya tangible things i.e. metaphysics kwa kweli nimeshindwa kuipata. Labda unisaidie.
 
Jambo ambalo lipo nje ya kanuni za physics naita ni uchawi.
 
Hakuna maisha baada ya kifo bali kuna maisha baada ya ufufuo.,

Haiwezekani mtu kuishi akiwa amekufa,na ili mtu huyo aishi ni mpaka afufuke tena
 
Jambo ambalo lipo nje ya kanuni za physics naita ni uchawi.

Umeandika kama vile kanuni za physics zimeshamaliza kuandikwa.

Kanuni za physics zenyewe bado zinagunduliwa, na nyingine ambazo zimegunduliwa tunaelewa kuzifanyia application vizuri.

Miaka 200 iliyopita kanuni za Einstein za Relativity zilikuwa hazijulikani. Je, hilo linamaanisha mtu angeona effect ya time dilation iliyosababisha mapacha wawili waliozaliwa siku moja, lakini kwa sababu ya time dilation mmoja akawa sawa na mzee wa miaka 90 wakati mwingine akiwa sawa na kijana mwenye miaka 20, angekuwa sawa kusema huo ni uchawi?

Watu wa Afrika waliokuwa hawajui kanuni za kutabiri kupatwa kwa jua (solar eclipse) walipokutana na wazungu waliojua kutabiri kupatwa kwa jua, kwa kutumia kanuni za physics, walisema kuwa hawa wazungu ni wachawi, ndiyo maana wameweza kutabiri kupatwa kwa jua, lakini hapo hakuna uchawi, ni kanuni za sayansi tu.

Sasa, wewe unaposema huu ni uchawi kwa sababu upo nje ya kanuni za physics, wakati hizo kanuni za physics zenyewe hujamaliza kuzijua, utajuaje huu ni uchawi kweli ulio nje ya kanuni za physics na si kitu kilicho katika kanuni za physics ambazo wewe huzijui tu?

Kwa mfano, tukichukua mtu ambaye yeye anajua kwamba kwa kanuni za physics kitu kizito ukikirusha juu lazima kianguke chini, mfano mtu aliyeishi miaka 200 iliyopita, tukamuonesha ndege ya Boeing 737 inaruka hewani kwa maelfu ya km bila kuanguka leo, kwa physics anayoijua, atasema huu ni uchawi tu, hili lidege likubwa zito haliwezi kupaa angani, kitu kizito hivyo kitaanguka tu. Lakini, kwa physics tunayoijua leo, tunajua ndege inaweza kuruka bila uchawi, sasa, na wewe utajuaje huu ni uchawi ulio nje ya physics na huu si uchawi ni physics nisiyoijua tu?

Na zaidi, utajuaje huu ni uchawi na si hadaa za watu tu? Kuna watu walikutwa wanacheza uchi nje ya gari Mombasa, walidaiwa kuwa ni wezi walioiba gari lililokuwa na uchawi wa kuwaondoa akili wezi watakaoliiba. Baadaye, uchunguzi wa polisi uligundua kuwa hapo hakuna uchawi wala nini, huo ni mchezo uliopangwa tu kati ya hao watu na mganga wa kienyeji aliyekuwa anatafuta promo.

Kwa jamii zetu, kuona watu wanacheza uchi ilikuwa ni kitu very convincing kwamba hapa kuna uchawi, lakini lilikuwa deal tu limepangwa na watu. Sasa wewe utahakikishaje unachoita uchawi ni uchawi kweli na si hadaa iliyopangwa na watu tu?
 
Hakuna maisha baada ya kifo bali kuna maisha baada ya ufufuo.,

Haiwezekani mtu kuishi akiwa amekufa,na ili mtu huyo aishi ni mpaka afufuke tena
Ufufuo ni nini na unahakikishaje kuwa upo kweli na si katika hadithi za uongo tu?
 
Ninaamini kwamba mm nina roho ila nzi na plasmodium hawana kwa sababu daima dumu wanaishi kwa mzunguko wa kimaisha (Life cycle)tu tangu enzi na enzi. Wanaishi, wanazaana then wanakufa. Hakuna badiliko lolote la maendeleo ktk mfumo wa maisha yao.
Wewe pia si unaisha unakufa unazaa why we unaroho ye hana
 
Mimi pia ni kiumbe hai kama yule paka anayetembea pale.ila nina cha ziada ambacho ni roho.

Oops! Verifiable evidence ya roho kwa maana ya tangible things i.e. metaphysics kwa kweli nimeshindwa kuipata. Labda unisaidie.
Unajuaje paka hana roho afu we unayo...
 
Mzee nakukubali kwa kujenga hoja.
 
Fanya research ndogo tu, tembelea vijiji kama Gamboshi
( Utakayoonyeshwa huko utajua kama ni kanuni mpya za physics, uchawi au vyovyote utakavyopenda wewe uite )


Wewe hauna data zozote kuhusu haya, Kwahiyo hauna haki ya kuzungumzia haya,
Kajifunze kwa faida yako sio yetu.
 
Sina haja ya kutembelea Gamboshi, tunaye mtu huko Gamboshi ni kwao yuko hapa anakwambia hizo habari za kwamba Gamboshi kuna uchawi ni hadithi za watu tu.

Yani kama wewe umeanza kuisikia Gamboshi ukubwani kwenye stories za vijiweni, yeye huko ndiko familia yake walipotokea.

Tatizo, ukishaanza na imani ya uchawi, ukiona story yoyote ambayo huna uhakika nayo, huielewi, haijathibitishwa, unaikubali kama uchawi.

Nimekuuliza, ukiona kitu ambacho unafikiri kipo nje ya kanuni za physics, utajuaje huu ni uchawi, na si kanuni za physics ambazo wewe huzielewi tu?Au hadaa za watu tu? Hujajibu maswali haya kabisa.

Haya ni maswali ya msingi sana, ukiacha kuyajibu unanionesha kwamba unabishana kishabiki, unatetea upande wako, huna nia ya kuchunguza mambo kwa kina na kupata ukweli.

Ama hivyo, ama huyaelewi maswali haya na umuhimu wake, jambo ambalo linanipa shaka sana kama mazungumzo na wewe yatakuwa na tija yoyote.

Unajuaje huu ni uchawi ulio nje ya kanuni za physics, na huu si uchawi, ni mambo yaliyo ndani ya kanuni za physics tu, kwa kanuni z aphysics ambazo sijazielewa bado? Hujajibu swali hili.

Unajuaje huu ni uchawi, na huu ni mchezo wa hadaa za walimwengu tu katika jitihada za kupambana na hali zao na kupigana pesa? Hujajibu swali hili.

Unaongelea data, huwezi kwenda kukusanya data bila ya kujua scope, bila kujua kipi kiko nje ya kanuni za physics na kipi kinaweza kuwa ndani lakini wewe hujazijua tu hizo kanuni.

Unakusanya vipi data wakati hujui hata mipaka ya kukusanya data iko wapi?

Unayaelewa haya maswali? Au unajibu kibishi tu kwa kutetea upande wako?

Nyani Ngabu
 
Wabongo wengi sana ukiwapelekea mchongo kamahuu, wanaamini kuwa ni uchawi kweli.


CCTV cameras reveal how Mombasa witchcraft stunt was staged – VIDEO​

By MOHAMED AHMEDSeptember 9th, 2017 2 min read



A CCTV footage has emerged showing how the witchcraft drama was stage managed in Bamburi, Mombasa.

The video clip, obtained by the Nation, shows one of the two alleged witch doctors arriving at the scene at around 6.30am with an unidentified man on a boda boda.

The unidentified man then pays the boda boda operator, who disappears from the scene.


The witch doctor, who was in a cowboy hat and a yellow t-shirt and was holding a black bag (believed to be carrying the snake), walks towards the alleged stolen car which arrived almost the same time he arrived.

After parking the Nissan Fugo beside the Bamburi-Mtambo road where the whole drama took place, the vehicle’s driver who is in a black t-shirt then walks away leaving the two alleged thieves in the car.

SNAKE

The witch doctor is then joined by the second purported sorcerer (Dr Tiachi) who are then seen walking past the car and disappear into an alley.

Minutes later, the two men (thieves), who have been identified as Patrick Omondi and Musa Ongomu, then come out of the car and start acting like a spell has been cast on them.


View: https://youtu.be/WNMdHo1fPMo
The two, who were both in their pants, then start doing what they did best as one is seen walking towards a pool of muddy water before he is joined by his partner.

One of them then walks back to the car and removes a snake from the black bag that was placed in the car by one of the witch doctors.

DRAMA

They then start undressing before residents start milling around them and taking videos of the drama which they only see on cinemas.

The revelation comes even as police said that the driver who parked the car before leaving the scene was among those being pursued as investigation continues.

“We saw what they did to deceive Kenyans. We will not allow this. We are going to arrest all those who planned that,” said Kisauni police boss Christopher Rotich.

On Wednesday, police arrested the four suspects for stage managing the incident were taken to court.

A fifth suspect, the woman Ms Elizabeth Sarah was also arraigned in a Shanzu Law Court where she pleaded guilty to giving false information to police.
 
Kifo ni kitendo cha roho kuacha mwili.

1.Kwani tukifa tunaenda wapi?

2.Kabla yakuzaliwa tulikuwa wapi?

Maswali haya 2 yanaonyesha huenda hawa watu 2 huwa kuna mahali wanakuwepo
 
Hili jibu unalitaka kwa mtu ambaye alishakufa / amekufa au anayeishi ? Kama unataka jibu kutokana na Imani za watu utaambiwa ndio; Lakini factual (what is known to be the truth) jibu ni hapana we are just a one specie of many, a part of ecosystem mbolea /.chakula cha species nyingine....
 
Huwa nikiona hizi stori za Gambosi kutoka kwa watu ambao nadhani hawajui hata hiyo Gambosi inafananaje, huwa nacheka sana.

Gambosi kumejaa umaskini lakini hizo stori zake sasa! Utaambiwa kuna ma sky scrapers, subways, viwanja vya ndege, high speed rails, na kila aina ya teknolojia mpya.

Cha ajabu, vyote hivyo havionekani. Ili kuviona, mpaka upewe ruhusa maalumu na wahusika wakuu!

Lakini ukienda kwenye nchi zingine, kuviona vitu kama hivyo wala huhitaji ruhusa maalumu toka kwa wahusika wakuu.

True story……nina ndugu ambaye alikuwa mgonjwa. Immediate family yake hawakutaka kumpeleka spitali hapo mwanzoni.

Wao walikuwa wanaamini kafanyiwa mchezo wa kichawi.

Wamezunguka kwa waganga wee, lakini hamna kitu.

Baadaye dakika za mwisho mwisho ndo wanaamua kumpeleka spitali ya Somanda, binti akafariki kwa BP!

Tokea mwanzo endapo wangeenda spitali, si ajabu binti angekuwa hai mpaka leo hii.

Yaani kuna watu wana imani za ajabu mpaka mtu unahoji uwezo wao wa kiakili.

Halafu sasa unakuta hata wale waliosoma na kuvuka nje ya mipaka ya Tanzania, baadhi yao wapo wanaoamini hayo mambo!

In my clan, for all I know, me and pops are the outliers. I haven’t met [and I haven’t met all of them] anyone else who doesn’t believe in that BS!

Sad.
 
Kifo ni kitendo cha roho kuacha mwili.

1.Kwani tukifa tunaenda wapi?

2.Kabla yakuzaliwa tulikuwa wapi?

Maswali haya 2 yanaonyesha huenda hawa watu 2 huwa kuna mahali wanakuwepo
Ukifa unaoza unakuwa mbolea ya mimea / hayo mafuta na nishati kadhaa almasi n.k. ni viumbe vilivyokufa zamani...

Kabla haujaziliwa ulikuwa haupo chanzo chako ni mbegu ni kama vile unashangaa huu muindi umetoka wapi wakati ulipanda mbegu / indi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…