Hivi kuna maisha baada ya kifo?

Haya kama sisi tunatakiwa kujibu hatujui kwasababu hatujajua dawa ya vidonda vya tumbo, wewe uhalali wa kusema ndio unaletwa na nini?
 
Kuna maisha baada ya kifo.

Atoms za mwili wako zitaendelea kuishi katika funza, mimea, etc.
Mkuu nimeuliza kuna maisha baada ya kifo,? Jibu ni ndiyo au hapana, kama ni ndio utatuambia umejuaje? Kama ni hapana nikwanini?
Kama utashindwa kuweka ndio au hapana huo ni uswahili.
 
Kuzimu ni wapi?
 
Maelezo meeeengi ila umeandika ujinga tupu, roho ni nini kwanza? Mbinguni je ni wapi, Mungu anakaa mbingu ya Saba ndio wapi huko!?[emoji53]
Unajua ni generation ngapi zimepita tokea generation ya Adam mpaka hii gen. yetu? Unaamini kabisa kizazi Cha Adam kinaendelea kusubiri kufufuliwa siku ya kiama! Ushavuta picha kwamba Kuna time itafika hiki kizazi chetu nacho kitakuja kuonekana ni 'zamani za kale' kama Cha enzi ya Adam tunavyokiwazia Sasa hivi. Hakuna kusubiri kufufuliwa sabab Dunia ipo na itaendelea kuwepo Haina mwisho
 
Mkuu nimeuliza kuna maisha baada ya kifo,? Jibu ni ndiyo au hapana, kama ni ndio utatuambia umejuaje? Kama ni hapana nikwanini?
Kama utashindwa kuweka ndio au hapana huo ni uswahili.
Sasa si nimekujibu ndiyo, nikakupa mfano wa funza na mimea, usichoelewa ni nini?
 
Au nikuulize maana ya kufa/kifo ni ipi?
Na mimi nikuulize maana ya maana ni nini?

Unapoandika neno "maana" unakusudia nini?

Neno hilo lina tafsiri nyingi tofauti zinazoweza kubadilisha jibu langu kulingana na unachokusudia.
 
Naam! Tuambie Mawazo unayahisi kivipi?
Tuachane na habari za Mahakama na mwenendo wa kesi zake turudi kwenye Hoja ya msingi kuhusu uwepo wa roho na kifo.
 
Acha utani watu wapo kwenye majadiliano.
Tabia ni nini?
1. Mkuu, Nami nachangia tu kama wengine katika majadiliano haya - sina utani. Kama nimekukwaza basi naomba unisamehe.
2. Mazoea hujenga Tabia. i.e. Kile kitendo unachofanya au kutenda kwa utaratibu fulani (kwa kujua au kutokujua) kila wakati ndicho kinampa mtu kuwa na Tabia fulani (Sifa fulani iliyojengeka ndani mwake)- nzuri au mabaya. e.g. Kila leo mtu anasema uongo na hata akigundulika na kuonywa habadiliki. Huyo watu husema anatabia ya kusema uongo i.e. Ni mwenye Tabia ya Uongo.
 
Hapana, hii research ilifanywa na nani? Kwamba mtu akifa roho inatengana na mwili?
Ndg. yangu katika mambo ya Imani ni nadra sana kupata Utafiti halisi wenye mashiko. Ni Imani tu.
Kama hauamini kile unachosoma vitabuni au kusikia kutoka kwa watu wenye Taaluma hiyo ni kazi bure. Unapoteza muda tu. e.g. Yupo jamaa aliitwa Thomas na katika mojawapo ya tafiti zake nyingi alikuwa akijaribu kuupata ufafanuzi muafaka wa Mungu mmoja katika Utatu. Kinachosemekana kilitokea kwake ni kwamba alimkuta mtoto akichota maji ufukweni mwa bahari kwa bidii sana. Thomas alimwuliza kulikoni na mtoto akajibu nataka nihamishie maji haya ya bahari yaingie katika shimo hili langu.
 
Sasa si nimekujibu ndiyo, nikakupa mfano wa funza na mimea, usichoelewa ni nini?
Okay basi sikuelewa kuwa hilo ndilo jibu linalomaanisha ndio,
Okay hawa wanaosema kuwa kuna maisha baada ya kifo ndicho wanachomaanisha? Au kila mmoja anajua kivyake?
 
Okay basi sikuelewa kuwa hilo ndilo jibu linalomaanisha ndio,
Okay hawa wanaosema kuwa kuna maisha baada ya kifo ndicho wanachomaanisha? Au kila mmoja anajua kivyake?
Wewe ulipouliza kama kuna maisha baada ya kifo ulimaanisha nini?
 
Okay basi sikuelewa kuwa hilo ndilo jibu linalomaanisha ndio,
Okay hawa wanaosema kuwa kuna maisha baada ya kifo ndicho wanachomaanisha? Au kila mmoja anajua kivyake?
Bibie kwa Kiranga hutoboi huyu ameshindikana jf nzima.
 
Na mimi nikuulize maana ya maana ni nini?

Unapoandika neno "maana" unakusudia nini?

Neno hilo lina tafsiri nyingi tofauti zinazoweza kubadilisha jibu langu kulingana na unachokusudia.
Nishaelewa je, nijamii yetu yote ndivyo inavyoelewa maana hii ?
 
Nishaelewa je, nijamii yetu yote ndivyo inavyoelewa maana hii ?
Jamii gani? Hiyo dhana yenyewe ya "jamii yetu" ni hadithi.

Hatuna jamii moja.

Mfano. Mimi Mtanzania. Nimelelewa na kusoma katika hiyo unayoiita "jamii yetu".

Lakini siamini katika Ukristo, siamini katika Uislamu, siamini dini za asili, siamini uchawi, siamini katika mimi kuendelea kuishi baada ya kifo. Siamininkwamba kuna roho.

Sasa imekuwaje mimi nikafika hapo licha ya kuzaliwa na kulelewa katika jamii hii inayoitwa yetu?

Na kama mimi nimeweza kuwa hivyo, unawezaje kusema jamii yetu yote ndivyo inavyoelewa maana hiyo?

Mimi ni sehemu ya jamii hiyo au si sehemu ya jamii hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…