Hivi kuna mashine ya kusongea ugali?

Nilikuwa naangalia documental NHK ya Japan jinsi Rice cooker ilivyogunduliwa/ilivyobuniwa nchini humo miaka ya 1950's.
Ilikuwa familia ya watu sita Baba,Mama na watoto wanne(4), Kutokana na Adha ya kuunguza chakula(wali)pale ambapo Mama anakuwa busy na shughuli nyingi za nyumbani, Baba wa familia kwa kushilikiana na mke wake walitafuta solution ya kupika chakula bila kuunguza.
Iliwabidi waunde kifaa kitacho warahisishia tatizo lao, Kwa utaalamu mdogo aliokuwa nao Baba wa famila alifanikiwa kutengeza plate ya hita(heater) na kuitenganisha na sufuria,tatizo likaendelea la wali kuungua, ikabidi atafutwe fundi wa umeme(Electrician) ndio alipo-suggest kuwekwa circuit breaker pale ambao jiko litaweza ku-maintain Hundred degree(100C), tatizo lingine likaibuka joto kupotea wali wali juu ulikuwa hauivi.Mama na Baba waka-give up hasa baada ya mama kuumwa,ndipo watoto wakaendelea na wenyewe Mzaee wao alipoishia, ila baba alipowaona watoto wanahaingaika ndipo alipo pata nguvu na kufanikiwa kuzuia kupotea kwa joto kwa kuzuia Joto kutoka nje, kwa mujibu wa hii documental walifanya majaribio ya maelefu na walichukia miaka.
Kwahiyo uvumbuzi wa Rice cooker ulikuwa wa kifamilia kwa ajiri ya kurahisisha suala la kupika chakula chao kikuu(ubwabwa), lakini kupitia uvumbuzi wao wameturahishia suala la kupika hasa sisi mabachela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…