Hivi kuna mbuga maeneo ya UDSM-Msewe-Baruti?

Hivi kuna mbuga maeneo ya UDSM-Msewe-Baruti?

KingCobra95

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
3,249
Reaction score
5,863
Kichwa cha habari kinahusika.

Katika pita pita zangu za hapa na pale, nimebahatika kupita maeneo tajwa hapo juu. Kwakweli sijawahi kuona utitiri wa ngedere kiasi hichi. Nakumbuka zamani hizo UDSM pale, tulikuwa tunawaona mara moja moja, lakini nilichokiona wiki hii, nilidhani niko Mikumi.

Mamlaka ya chuo hebu shirikianeni na madiwani wa maeneo ya karibu hayo mfanye mpango muwa-castrate au muwaombe Tanapa wawasaidie maana muda si mrefu wataanzisha koo karibia na barabara ya Morogoro.

Ndio dukuduku langu.
 
Mkuu kwani lile pori chini pale hulioni wameacha kama kivutio. Nimewinda sana ndege na sungura kwenye lile pori.
 
Sasa vingedere vya Mungu vina shida gani na wewe?
 
Wanachuo wanafurahia kuwaonaa hao ngederee waachwe.
 
Wale hawanaga madhara kabisa hadi darasani huwa wanaingia kukiwa na utulivu sana. Ila huwa wanadharau kwa mtu asiyekuwa na hela, hata umfukuze hakimbii bali anatembea tu coz anajua huna cha kumfanya umeishiwa.
 
Back
Top Bottom