Hivi kuna mchawi anaweza kufungua password ya iphone kiuchawi?

hazole1

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
4,319
Reaction score
3,916
watu wanavyo wasifia wachawi inaonekana wachawi ni watu wenye uwezo mkubwa sana.

nasikia kuna waganga wengine ukienda Kwake anakuambia usimuambie matatizo yako.yeye ndio anaanza kukuambia.
jina lako unaitwa nani na tatizo gani lililokupeleka kwake.

na akishatoka hapo anaanza kukuonyesha hadi adui yako live kwenye kioo.

kwa maelezo hayo nikajiuliza swali moja.
mbona mwaka jana FBI walihangaika sana kufungua password ya
simu ya iPhone. na walitangaza dau lefu kwamba atakaye itoa wanamuachia mkwanja wa kutosha.

na nikajiuliza kwanini mchawi hata mmoja hakujitokeza kwamba anaweza akaitoa hiyo password. na hiyo ilkuwa ni fulsa nzuri kwa wachawi wote na ingewasaidia wachawi kujitangaza kwamba nao wapo na wanaweza.

na niliwaza nilifika Mbali sana na nikajiuliza hivi hata humu jf hamna hata mchawi mmoja ambaye angeweza kufungua hiyo password kiuchawi.
hadi ile simu ikaenda kufungilwa Israel.
 
ha ha! kwangu ni kama mastori fulani hivi yakupita!
uchawi na teknolojia wapi na wapi ndo yaleyale ya kwenye vita vya majimaji walitusuliwa na imani yao yakichawi...
 
ila vinachanganya kwakweli, hasahasa wale watu wanaopandisha mashetani,
na hata wale wanaofanya mazingaombwe, huwa wanafanya kwa nguvu za kitu gani ndani yao?
 
Ushawahi kuona mchawi tajiri?

Kama ni tajiri sio mchawi ila ana mali za uganga au majini na yeye sio mchawi ila anajua ndumba kwa maelekezo maalumu.

Ukipata jibu hilo njoo tuendelee na tafakuri..
 
ha ha! kwangu ni kama mastori fulani hivi yakupita!
uchawi na teknolojia wapi na wapi ndo yaleyale ya kwenye vita vya majimaji walitusuliwa na imani yao yakichawi...
wale wanasema uchawi upo tunataka watuthibishie kwa hili la password
 
Kuna jamaa mtoa topic za uchawi aje atuambie ni kwanini hilo linashindikana
 

= refu
= fursa

Unadhihirisha kuwa shule ulienda kusomea ujinga.
 
Mchawi adui yake ni utajiri mbona wanaingia ndani ya nyumba kiuchawi hawachukui pesa zipo juu ya meza.hivi uchawi faida yake nini?
Una uhakika kama wanaingia ndani? Nani kawahi kuwaona?
 
Wachawi wangekuwa na akili mimi ninatamani wangechapa viongozi bakora kila wakifanya kinyume ila MICHAWI YETU IPO TU KUUWA WALE WANALETA MAENDELEO,wanataka watu wote wawe masikini.

Wachawi wa Tanzania mnakera sana
 
Uwezi uchawi kitu cha kienyeji ni tofauti na technology ingekua hivyo uchawi si ungeweza kutoa fedha kwenye ATM zote za mini na kufuta kumbukumbu zote za kibenki
 
Uchawi hauwezi shindana na technology, ni nguvu dhaifu ungekuwa na nguvu ungetumika kuzuia Africa isitawaliwe au kuzuia watu kuchukuliwa utumwani,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…