Umeelewa swali langu?
NAKURAHISISHIA:Ile orodha ya Mwembeyanga ilikuwa ya mafisadi au siyo mafisadi?
Halafu naona umekomaa na Richmond pekee,kwa taarifa yako Lowassa mlimtaja fisadi kabla ya Richmond.
Ilikuwa orodha ya watuhumiwa wa ufisadi na si mafisadi. Lowassa ameshasema yeye hausiki na mhusika ni Kikwete. Hivyo Lowassa anatolewa rasmi kwenye listi ile ya watuhumiwa na mtuhumiwa hapa ni Kikwete.
Hata kwenye kutajwa kwa Lowassa kwenye maeneo mengine ukiacha Richmond bado ni kumtuhumu tu. Serikali iliyokuwepo madarakani wakati huo ilikuwa na jukumu la kumburuta mahakamani ili ajibu tuhuma kama zilikuwa na ushahidi wa uhusika wake kwenye matukio hayo. Kwa nini haikufanya hivyo?
Kama kweli Lowassa alihusika katika wizi anaoutuhumiwa, basi Serikali ya wakati huo nao ni wezi kwa kushindwa kumchukulia hatua kama walikuwa na ushahidi kwa sababu huwezi kumuacha mtu anaiibia Serikali mabilioni ya pesa bila kuchukua hatua yoyote kama wewe mwenyewe sio mwizi.
Sasa kwa issue ya Magufuli hii iko wazi kabisa kwamba kuna ushahidi wa kitaalam uliotolewa na CAG kwamba alitunga mradi hewa wa ujenzi wa barabara na kuupatia namba hewa ili kuiba mabilioni ya walipa kodi.
Inaingia akilini namna gani mtu ambaye amethibitishwa kuwa mwizi wa mali ya umma aliyekubuhu kwa kudanga mradi pamoja na namba ya mradi ndio huyo CCM inatuletea eti tumpigie kura ya kuwa Rais wa Tanzanina?
Kama aliweza kuiba mabilioni wakati akiwa waziri, ni wazi kwamba ataiba matrilioni akiwa rais tena bila kutunga uongo wa kuhalalisha wizi wake bali atakwapua mchana kweupe bila justification yoyote ile hata ya uongo.
Kwa nini CCM watuletee mwizi aliyekubuhu kwenye kinyang'anyiro cha mgombea urais? Bila shaka ni kwa sababu waliompigia debe ili agombee ni wezi wenzake ili waendelee kuliibia taifa hili kupitia mgongo wa mwizi mwenzao atakapoingia ikulu.
Watanzania mumuogope Magufuli kama Ebola ama sivyo nchi itafilisiwa kabisa katika kipindi chake cha mwaka mmoja tu.