Hivi kuna muda au umri wa kuoa au kuolewa?

Hivi kuna muda au umri wa kuoa au kuolewa?

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
545
Reaction score
1,179
Habari JF,

Wakuu naomba ufafanuzi mdogo hivi kuna umri flani ukifika inabidi kuoa au kuolewa, yaani kuna muda inabidi uwe kwenye ndoa. Na je, ni umri gani?

Na hii ni kwa dunia nzima au? Utakuta mtu bado maisha yako mwenyewe peke yako ujiwezi wazee na majirani wakija kila siku wanaulizia huyu kijana wako ajaoa tu umri huu ebu fanyeni mumuozeshe.

Sasa nawaza kuoa au kuolewa ni inaenda na muda au mpaka mtu uwe umejiandaa kimaisha kuwa na familia.
 
Maranyingi kuoa au kuolewa ni kipaumbele cha mtu.

Unapoamua kuingia katika huo mpango lazima unamambo yako unataka hivyo mahitaji ya watu hayalingani kutokana na umri wao. Mfano kuna jamii ukimalizatu darasa la saba unaoa au kuolewa wakati wengine mpaka wamalize degree, wengine mpaka wajenge na wengine mpaka wanunue vipando

Maranyingi kuoa hakuna umri maalum bali mtazamo wa jamii na msimamo wa mtu
 
Kuoa au kuolewa ,
Ni makubaliano ya wawili wapendanao walio ridhia kuishi pamoja katika Kila hali ikiwa tu umri una ruhusu,
 
Kwa kawaida inabd ukifika miaka 18 inabd uoe au kuolewa sema ni vile tunakuwa shule au maisha hayajanyooka


Ilaa vyote vingekuwa sawaa huu ndo umri sahihi ili tuzae tulee watoto mapema ingali bado tuna nguvu .angalia wanao oa au kuolewa wakiwa na 30 + MTU mpaka anafika 60+ plus bado anasomesha na kulea watoto
 
VP wa Marekani aliolewa akiwa na miaka 51.
Juzi juzi tulimuona Juma K akioa kabinti ka 25 aka Dada Mwaju.
Kuna mpaka mawaziri hawajaolewa pia mabaameid wengi hawajaolewa.
 
VP wa Marekani aliolewa akiwa na miaka 51.
Juzi juzi tulimuona Juma K akioa kabinti ka 25 aka Dada Mwaju.
Kuna mpaka mawaziri hawajaolewa pia mabaameid wengi hawajaolewa.
Hahaha nimecheka hapo kwa ma baameid
 
Habari JF,

Wakuu naomba ufafanuzi mdogo hivi kuna umri flani ukifika inabidi kuoa au kuolewa, yaani kuna muda inabidi uwe kwenye ndoa. Na je, ni umri gani?

Na hii ni kwa dunia nzima au? Utakuta mtu bado maisha yako mwenyewe peke yako ujiwezi wazee na majirani wakija kila siku wanaulizia huyu kijana wako ajaoa tu umri huu ebu fanyeni mumuozeshe.

Sasa nawaza kuoa au kuolewa ni inaenda na muda au mpaka mtu uwe umejiandaa kimaisha kuwa na familia.
Umri auhusiki

Wewe uwe tayari

Hata usipooa sawa tu, kwani Yesu alioa???

Usifate mkumbo

ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO
 
Mi nahisi hata mwili wenyewe unasemaga hapa jamani I need samsing ama nitaharibikiwa.

Kuna ka alarm kanaitaga ka kutamani mwenzako wa kutulia nae sio tu kukulana kimasikhara.
 
Back
Top Bottom