Hivi kuna mwanaume aliyewahi kumpa mpenzi wake biashara halafu ikafanikiwa?

Akilitime

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2017
Posts
581
Reaction score
758
Kama umewahi kumpa biashara mpenzi wako ili aisimamie , na ikafanikiwa tuambie ulitumia njia zipi,
Pia wewe aliyeishia kupotezewa hela yako tuambie ilikuwaje,
Mwisho unatoa ushauri gani kwa vijana wenye wapenzi
 
Sijawahi ila nimeshashuhudia watu 2 tofauti.
Hizi biasha huishia
1. Kufirisika au
2. Conflict kati ya mke na mume au mtu na gf wake.

Chanzo hasa huwa ni ;
1. Matumizi mabaya ya pesa
2. Wivu wa kimapenzi
3. Mke au gf kuanza kujiona Super power kwa mume au bf wake.

Tusubirie comments za wadau.
 
Mwanamke muache a fight mwenyewe kwanza. Ukiona ana bidii na anafanya kwa dhati pia kuna hatua japo kidogo kwenye anachofanya ndio sasa jifunze juu ya anachofanya na ujue jinsi ya kumuongezea nguvu.

Hii mnapiga stori chumbani ...baby nikufungulie biashara gani ....utaishia kutajiwa tu zile common business ili mradi anaona mastaa wanafanya huko Instagram na si mpango na ndoto zake. Otherwise mtaishia kuwalaumu kwa mitaji kufa.
 
Kuna ndugu mmoja kampa mkewe mtaji wa million 15 akawa anauza gas, matokeo yake kila akipata hela anatumbua na mashoga zake. Mikopo kila mahali mpaka kwenye WAWATA kiasi kuwa mume akitoka kanisani hajui hili wala lile anakabwa na akina mama.

Kawaambia wamfunge kama wanataka atajua mwenyewe. Imagine wanaishi ndani lakini hawasemeshani kisa ujinga wa mke.

Kama upo humu nisamehe mmama.
 
Bahati NZURI kwetu hakuna MADEMU, kuna wanawake tu tena wanaojitambua vyema.
Mleta mada anauliza kuhusu DEMU/MPENZI, sasa hao wanawake wa kwenu "wanaejitambua vyema" watakuwa labda hawapendeki hivyo hawana sifa za kuitwa MPENZI.
(usikasirike lakini)
 
Mleta mada anauliza kuhusu DEMU/MPENZI, sasa hao wanawake wa kwenu "wanaejitambua vyemna" watakuwa labda hawapendeki hivyo hawana sifa za kuitwa MPENZI.
(usikasirike lakini)
hakuna mwanaume mwenye akili timamu atamuita MPENZI wake DEMU.
 
Mkuu, mimi nilimpa Mwaju Nichokonoe mtaji wa kuuza vitumbua pale buguruni....
Leo Mwajuma nichokonoe anasukuma ndiga na kubadilisha biashara kutoka kwenye vitumbua hadi electronics resources
 
Mkuu, mimi nilimpa Mwaju Nichokonoe mtaji wa kuuza vitumbua pale buguruni....
Leo Mwajuma nichokonoe anasukuma ndiga na kubadilisha biashara kutoka kwenye vitumbua hadi electronics resources
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Huyu mwaju nichokonoe leo lazima atacholewa.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Huyu mwaju nichokonoe leo lazima atacholewa.
[emoji14] [emoji14] [emoji13] [emoji13] [emoji12] [emoji12]
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Kumbe bora kila mtu apambane kivyake tu
 
Hakuna na wengi hawana akili za kurun biashara atatia hasara na bado wew ndio utaambiwa ujazie mtaji biashara isife........
Kama wapo ni mmoja kwenye kumi
 
Mshikaji wangu alifilisiwa chumba kizima kisa mkewe kumtia kwenye madeni yasiyoeleweka
 
Mkuu, mimi nilimpa Mwaju Nichokonoe mtaji wa kuuza vitumbua pale buguruni....
Leo Mwajuma nichokonoe anasukuma ndiga na kubadilisha biashara kutoka kwenye vitumbua hadi electronics resources
Mkuu safi sana,Maana watu wamezoea negativity kila kitu.Hata na mimi pia nimempa mrs Nguvu sio Pesa mtaji ni kama miezi 8 sasa imepita.Pesa yangu kanirudishia na mambo yanakwenda fresh
 
Kama umewahi kumpa biashara mpenzi wako ili aisimamie , na ikafanikiwa tuambie ulitumia njia zipi,
Pia wewe aliyeishia kupotezewa hela yako tuambie ilikuwaje,
Mwisho unatoa ushauri gani kwa vijana wenye wapenzi
Kwanza unamfungulia mwanamke ambaye kiuhalisia sio ndugu yako wa damu ke utakua na akili timamu?

Unamfungulia mwanamke biashara kwann usiwafungulie wale wadogo zako kule kijijini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…