Hivi kuna nini tigo mbona kupata tigo pesa uwakala ni shida sana?

Hivi kuna nini tigo mbona kupata tigo pesa uwakala ni shida sana?

Mbwambo

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
625
Reaction score
94
Jamani wapendwa naomba mtu anayeweza kunisaidia kuniunganisha na mtu tigo ili nipate uwakala wa tigo pesa.
Nimekwenda mahali fulani nikaacha hela yangu tshs. I million kwa miezi kadhaa kila siku naambiwa leo kesho njoo leo kesho njoo mpaka nikashindwa nikaomba nirudishiwe hela yangu.

Nimerudishiwa hela yangu ila sasa naomba msaada kwa yeyote maana wateja wengi sana kuliko mpesa ambayo ndiyo nilipata ki-ulaini tu.

Asanteni wana jamii forums
mama yenu na mwanachama mwenzenu
 
Laki moja. Temporary hadi yakwako iwe tayari.
 
du hata mimi nimeacha hela hapo sijui nichukue maana huu unaenda mwezi wa pili sasa
 
du hata mimi nimeacha hela hapo sijui nichukue maana huu unaenda mwezi wa pili sasa
 
rushwa ni adui wa haki lakini hapa bila rushwa mizengwe mingi
 
Laki moja. Temporary hadi yakwako iwe tayari.

Kaka Mbona sijakuelewa ukisema Laki Moja? Ina maana mpaka nitoe LAki moja kwanza kisha ndio nisubiri ya kwangu naomba nisaidie hata kama utaweza nitumie kwa private message
Asante
 
me mwenyewe hadi nimemaliza soli za viatu kwenye relini pale,ni zaid ya miezi miwili imekata.Naelekea kukata tamaa niombe kurejeshewa hela yangu kama wewe
 
Mnanikumbusha nilipokuwa natafuta uwakala wa mpesa tangu mwaka jana mwezi wa nane, nikapata mwezi wa nane mwaka huu tena kwa mbinde sana! Na sikuwapa hata senti kumi yangu.
 
mnanikumbusha nilipokuwa natafuta uwakala wa mpesa tangu mwaka jana mwezi wa nane, nikapata mwezi wa nane mwaka huu tena kwa mbinde sana! Na sikuwapa hata senti kumi yangu.

sasa naona kila mahali ni tofauti. Mimi voda nimekwenda kwa happy mvungi siku moja nikaambiwa nilete vitu vinavyotakiwa nikawapelekea. Huwezi amini siku hiyo ninaambiwa niende kesho yake nikapewa line. Kwahiyo sikuwekewa hata mazingira ya kuonyesha wanataka pesa hata kwa ufupi baada ya siku tatu nikapewa line ya mpesa.
Sasa nashangaa wengine wanasema wamesota mpesa?
 
hizi line zinapatikana lakini kwa kutoa pesa mimi kuna jamaa yangu katoa laki 2 kapewa bila kuombwa tin number wala chochote
 
hizi line zinapatikana lakini kwa kutoa pesa mimi kuna jamaa yangu katoa laki 2 kapewa bila kuombwa tin number wala chochote

jamani mbona kazi sana yaani laki mbili nitoe ndio nipate line ya uwakala?
Kaazi kweli kweli jamani
 
jamani mbona kazi sana yaani laki mbili nitoe ndio nipate line ya uwakala?
Kaazi kweli kweli jamani

...Kaazi kweli kweli yaani! Nilidhani wao ndio wangepaswa kubembeleza watu kuwa maagent wa huduma zao kumbe sisi ndio inabidi tuwalambe miguu ili tuwaingizie fedha!! Nchi hii inekuwa na Umoja basi ilikuwani kiasi cha kuwagomea tu laini zao na ungeona jinsi ambavyo wangetubembele kuzinunua, lakini ndio hivyo tena! wabongo tumo kwenye usingizimzito wa kutojua haki zetu!!
 
Back
Top Bottom