Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
- Thread starter
-
- #21
Biashara unajua kabisa nachukua mahindi Mbeya kwa 6000 debe naenda kuuza dar 10000 debe. Unapiga gharama ya usafiri unajua na faida yako. Kwenye Hisa unabet kuwa labda jinsi uchumi unavyoenda basi hisa za FB zitapanda. Unanunua ili uuze kwa faida, ila huna hakika. Kwenye Fx unaangalia uchumi wa nchi na matukio kucheki kupanda na kushuka kwa pesa unaenda na hizo taarifa kufanya business ila huna hakika itapanda kiasi gani au itakuwaje na inaweza isiwe hivyo kabisa.Biashara gani ina faida ya uhakika moja kwa moja??
Hata kwenye kubet mpira watu wanacheki vikosi, nani yuko nyumbani, majeruhi, umuhimu wa game, nani anajua kujilinda, nani anafunga sana nk. kisha anatumia hizo taarifa kuweka mkeka. hizi mambo zinafanana sana. Tofauti na mtu anayenunua mashati China na kuja kuuza Bongo. Anajua kabisa ataauza kiasi gani na atapata faida kiasi gani. Ukienda na hela ndogo anakwambia hailipi.