Watasifiwa panapostahili....kila mtu kwa nafasi yake. Ila kuwapenda wote mmmmhh.....lazima tu kutakuwa na mmoja unayemkubali zaidi!
As for me, Diamond yuko juu sana kimafanikio na kiasi fulani amefanikiwa kuliteka soko la kimataifa but when it comes to taste dah Alli K is my taste bhana.....nyimbo zake zinanikosa sana. The dude knows how to sing aseee!! Kwangu mimi hakunaga kama Kiba He is my favourite!!
Ila sasa tukibadili kidogo aina ya muziki ndo tunakutana na wakali wao Banana Zorro na Christian Bella......hawa nao mziki wao si mchezo yaani!
Ila tatizo kubwa lililoko kwetu sie mashabiki ni zile elements za unafiki. Kuna watu kazi yao ni kuponda tu hata pasipostahili. Unakuta mtu kama hamkubali msanii flani aidha Diamond au Kiba....basi lolote litakalozungumziwa kuhusu huyo msanii haijalishi ni jema ama baya, yeye ataponda tuu kwa nguvu zake zote na ikitokea mwingine akasifia basi inakuwa shida mara mia nane ka si ugomvi kabisa!! Likewise.....unakuta mtu anamkubali either of the artists.....basi lolote litakalozungumzwa juu yake, yeye atasifia tuuu kwa nguvu zote hata kama msanii msanii kabolonga ama kafanya jambo ambalo hakustahili sifa nzuri......sasa kimbembe mtu mwingine atokee amkosoe hapo inakuwa ni ugomvi tena kama si mtu kuambiwa ana wivu!!
Anyways....si mbaya tukakosoa ama kusifia panapostahili haijalishi we ni shabiki namba moja au namba ziro. Na wale wasopenda msanii wao mpendwa akosolewa basi hao hawafai na ndo wachonganishi nambari wani probably hawawatakii mema wasanii wao as huwa wanamuatack kila anayejaribu kutoa kasoro!!