Ni kwasababu mwenye asili ya jina hilo (Mwenye jina lake) ni mtu ambae aliukubali uisilamu kwa kutumia ELIMU (KITABU), anaitwa
Omar bin Khatab alikuwa ni mtawala wa Tatu katika uisilamu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w), asili ya familia yake inatokna na kabila la Kikureish. Katika ujana wake Omar alikuwa maarufu ktk upiganaji. Omar (r.a) alikuwa ni miongoni mwa watu wachache waliokuwa wanajuwa kusoma na kuandika ktk Mji wa Makka kabla ya kuja Uislam .
Umar alikuwa ni adui mkubwa wa Uislam na Mtume wake (s.a.w).
Kuslimu kwa Omar bin Khattab (r.a) hapa ndipo kwenye asili kwanini kina Omar ni waalimu na wasomi wazuri
Omar aliiñgia ktk Uislam mwaka wa sita baada ya Utume. Mwaka huo viongozi wa Kikureish waliweka mkutano wa kutafuta mtu atakayejitolea kumuua Mtume Muhammad s.a.w . Omar alisimama na kusema yeye ni mtu sahihi wa kufanya kazi hiyo.
Wakati yuko njiani akiwa na panga alikutana na mtu anaitwa Sa'ad bin Abii Waqas . Omar alimwambia Sa'ad "nakwenda kumuu Mtume s.a.w . Baada ya majadiliano Sa'ad alisema " Kwanza unapaswa kushuhulikia familia yako na pia Dada yako na Shemeji yako wameshasilimu"
Baada ya Omar (r.a) kusia vile alibadilisha mwelekeo wake na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Dada yake (Fatma). Wakati huo Omar anagonga mlango walikuwa wanafundishwa Qur'an na Khabbab (r.a).
Dada yake alishtushwa na sauti ya Omar . Baada ya Omar kuingia ndani aligundua kuwa kweli wameslimu. Hapo hapo akaenda kumshambulia Shemej yake na kumpiga. Dada yake alipotaka kuingilia kati alimshambulia na kudondoka na akawa anatoka damu ktk uso wake .
Fatma alisema "Fanya utakavofanya sisi tumeshaingia ktk uislam na tutakufa ktk Uislam" Mara Omari alimuona Dada yake anatoka damu ktk uso wake alijiskia aibu na huruma kwasbabu alimpenda sana Dada yake .
Hapo hapo Omari alimwambia "Nifungulie Qur'an lakini Dada yake alimwambia huwezi kugusa Masahaf mpaka utie udhu " . Omar alikoga na kutia Udhu . Baada ya hapo Fatma alimfungulia Surat Twaha (20:14 ). Fatma alisoma kwa sauti aya ilikuwa inaeleza .........Mimi Mungu na hakuna Mungu ...........(20:14)
Omar alisema ni kweli haya ni maneno ya Allah nipeleke kwa Muhammad s.a.w . Baada ya kuskia vile Khabbab r.a alisema dua ya Mtume s.a.w aliyoimba usiku wa jana yake imejibiwa na Allah .. Mtume s.a.w aliomba kuwa Omar bin Khattab or Omar bin Hisham mmoja wao asilimu awe muislam .
Omar (r.a) alipofika kwa Mtume s.a.w alimwambia umekuja kufanya nini Yaa Omar ?. Omar alisema "Nimekuja hapa kuslim. Maswahaba waliokuwepo kwa pamoja walisema Allah Akbar .
Kuslimu kwa Omar kuliwahuzunisha na kuwasononesha Makurwish wa Makkah hii ni kutokana na nguvu na kukubalika ktk mji wa Makkah
Abdallah bin Masuud alikuwepo pale na akasema " kuslimu kwa Omar ni Ushindi kwa Uislam " . Na ni kweli kabisa baada ya Omar kuingia ktk Uislam Uislam ulipata nguvu kwsbb watu wengi walislim baada ya kufahamu ukweli juu ya Uislam.
Maana ya jina OMAR, ni kustawi au kuishi kwa muda mrefu. (Kumbuka watu wanakufa lakini elimu huwa haifi). (Mashariki ya Kati) Omar, Omer, Ömer, Umer au Umar (Kiarabu: عمر), ni jina la kiume, ambalo linawakilishwa katika mila ya Kiyahudi, Kikristo na Kiisilamu.