Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Kaka,huyo shemeji yako nilishamuacha kitambo,kuwa maskini hakukatazwi as long as unapambana inaonyesha Nia ya kuuchukia umaskini,Ipo siku Mungu atakukumbuka.Tatizo Ni kuwa na mtu asiyejituma Wala kujiongeza,hapa tunatokaje sasa...Hapana hapa tunamsingizia shetani.
 
Mkuu nipe connection ya kuja mbele mkuu. Kila kitu lipo tatizo documents
 
Ooooh kesi ya huyu mtu sitoiweza....labda tu angesaidia kutuelezea kwa nini huwa warudi Kama walivyoenda?
Si wote!! ni sawa na mtu kutoka Mkoa!! wengine hawatamaniga tena hata kurudi na kuishi Dar! kwa jinsi wanavo pigika ! mfano mzuri ni km binamu yangu Aloyce yeye alirudi Mkoani kwao kijijini na gari zile zinazo sindikizaga Mahiti kwa maana kuwa

hakuwa na hela kabisaa hata Nauri ya kumrudisha home kwao...... watu km hawa wanaona Dar ni Bonge la gereza waepuke km ukoma, na wengine ndo kwaanza, wanapeta ni ile mbaya, wanasoma kirahisi na kupata kazi safi! na wanajenga mijengo ya maana.

hawa usiwapuuze jifunze kwa hawa!! Ughaibuni pia ivoivo!...kunawengine hawana bahati huko,na kuna wengine wanabahatika huko kwa kumweka Mungu mbele! wengi tu wapo wanarudiga huko kuoa/kuolewa tu!

Mifano ya wakubwa km hao ipo miiingi sana hapo Bongo mmoja wao akiwa ni january makamba huyu alirudi tu lkn alikuwa na Ulaji wa kutosha majuu.....Marwa winani, Dandu, nk
 
Yaani hapo unawapa assuarance kwamba hela unayo sema tu kuna mission unaisikilizia,Yaani kitendo cha kusema umefika New york ni CV mama
🀣🀣🀣🀣🀣🀣Wanapenda hiyo Kuna hela wanaisikilizia,utasema yake mabilioni ya Doctor Shika...R.I.P
 
Ni kweli,Soma Uzi tumesema wachache wanafanikiwa Ila majority wanaorudi hoi.
 
Ni kweli,Soma Uzi tumesema wachache wanafanikiwa Ila majority wanaorudi hoi.
Uko sahihi! lkn nakushauri kaza uzi palee karoho kako kanapenda!! roho yako ni Mtumishi Mwaminifu haiwezi kukudanganya kamwe hii ndo siri pekee nakupa!.....ni km mie .karoho kaliniripuka nikabeba house girl kabisaaa! kutoka kwa shangazi yangu nilipokuja likizo hapo Bongo!!

Lkn huyo aligundua fursa nyingi huku!! ambazo sikuwahi zifikiria, kasoma weee! na sasa ame specialize kozi flani hivi namshukuru sana shangazi yangu! alinisisitiza ''huyu ndo mke chukua ndo akaua kabisaa'' kupitia uzoefu huo, bila uchoyo na mie nakushauri ivo ivo!

km jamaa moyo ulikuripuka siku hiyo mwana wee kamatia tu!... tena mume wakuanza nae moja ndo bomba usisikie!!! atakuachia wapi wkt umeanza nae kulala chini? akifikiria alivokuwa mlevi kwishne anajirudi...

komaa mwana usiachie!!! hilo nitakusisitiza tu! popote pale ntapo kutana na wewe!! iwe kwenye ndege, daladala,sijui Hosp, mie ni komaaa tu! baasi!

sikia sasa Ughaibuni siyo wachache wanafanikiwa big no!....... wengi wanafanikiwa!! hawa kundi hili huwaoni kabisaa wako Matawi fiche!! .....shetani siku zote anakuonyesha life failures!! tena ni mjanja sana!

(Funga nakuomba kwa imani ya Dini yako! hakika utaona njia,... Mungu ni Mwaminifu zaidi ya Uaminifu sijawahi ona!!)
 
Me napenda kujua watu mlioenda Huko majuu ulaya mtupe kidogo mawazo mkifika kwa mara ya kwanza hali ikoje kuhusu vyakula ? Vp gharama zikoje? , kuna mama ntilie ? Mtu anaweza kupata vyakula kama vya huku Bongo mfano maharage , mlenda , ugali n.k ?

Siku nikifika Dar , naamini pia nitafika Ulaya.
 
Yaani unazungumzia matabaka gani, sisi tunachoangalia kule kuna kazi nyingi na fursa nyingi, malipo ni makubwa si ndio? Kukomaa kwa matabaka kunatuhusu nini, mtu kapata kazi kiwandani anagonga mzigo!
Huku afrika pia kuna matabaka na ukabila,tafuteni maisha msikatishwe tamaa na wajinga
 

Nje vyakula vyote vipo yani vyote from magimbi to mlenda to dagaa tofauti inaweza kuwa ladha tu ila vyakula unapata. Mnajua vyakula vingi ambavyo leo mnaona ni vyetu vimetoka nje; mchele ulitoka Asia, magimbi na parachichi S. America nk
 
Umefanya generalization sana.

Sample yako bado ndogo sana kuprove uhalisia wa kizungumzwacho.

Wengine tuna miaka 20 + sasa na hakuna tofauti maisha yanakwenda vizuri na 2016 ndio sikufikiria kurudi nyumbani baada ya kuamua kuchukua uraia wa huku kabisa.
 
Huko mbali mnakofika wapi? Kupata ajira ya 1/2m, kununua RAV4 ya miaka 15 iliopita na kujenga Goba huko? Kila siku humu watu wanalia maisha magumu Tz leo hii mmefika mbaaali!
Sasa mkuu we unadhani mtu mwenye maisha magumu Tz atakuwa na maisha mazuri akienda huko Ulaya Marekani etc?
Mtu anapigwa na maisha hapa Tz je huko? Si yatamua kabisa?
 
Unazingatia dini sheikh Allah akulipe wengi hubadilika wanapohama mazingira wanayoishi na kuitelekeza dini .....ungejibanza nchi za kiarabu kule au Turkey.

Waarabu wenyewe wanazamia Ulaya na NA. Ushawahi ona mtu anatoka nchi za ME au North Africa au Somalia anataka kwenda arabuni? Wanazikandia wakiwa kwao ila Wote wanataka Kuja kiwanja Mzee. Kiwanja is where it's at.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…