Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Wasalaam wanajamvi.

Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.

My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.
Ulaya watu hawajengi nyumba wewe. Kwako kujenga nyumba ndiyo kipimo cha maendeleo. Kuna Watanzania wengi sana wanaishi KIHALALI na wana maisha mazuri sana Ulaya na Marekani na hawana mpango kabisa wa kurudi Tanzania ever!
 
jamaa ninaowafahamu wengi walizamia kwenda nje wengi walikaa south sana then kutafuta viwanja kama uk, italy ,sweden,denmark
wamefanikiwa baadhi na ni wengi wale wanaojitambua wameshusha mijengo, magari ya biashara

wawili waliofeli walitoka wavuta bangi wamerudi wanaconsume mpaka unga balaa tu wamekuwa matej na matattos kibao hawana mbele wa nyuma hawa ni wachache kuna kama wanne wametusua wameoa tena wamekuwa ni watu wa dini sana wanatoa misaada

siri hao mateja wote huku bongo kwao sio haba na waliacha shule za ghali wakenda huko wana asili wa uarabu shombe shombe nguo tu wanazo za kutosha ila saa 7 mchana jua kali unakuta wametinga
 
Hatuongelei kujenga nyumba ulaya wewe!acha kuparamia treni kwa mbele tulia Soma uelewe ndio urudi kutoa hoja hapa
 
Hatuongelei kujenga nyumba ulaya wewe!acha kuparamia treni kwa mbele tulia Soma uelewe ndio urudi kutoa hoja hapa
Wewe exposure yako na diaspora ni failures wawili watatu wa Tangi bovu? You don't know shit. Hata Dubai inawezekana hujafika. Umekuwa disappointed na BF wako aliyekuwa anaishi Ujerumani ulitegemea angekuoa mkaishi wote Ujerumani.
 
jamaa ninaowafahamu wengi walizamia kwenda nje wengi walikaa south sana then kutafuta viwanja kama uk, italy ,sweden,denmark
wamefanikiwa baadhi na ni wengi wale wanaojitambua wameshusha mijengo, magari ya biashara

wawili waliofeli walitoka wavuta bangi wamerudi wanaconsume mpaka unga balaa tu wamekuwa matej na matattos kibao hawana mbele wa nyuma hawa ni wachache kuna kama wanne wametusua wameoa tena wamekuwa ni watu wa dini sana wanatoa misaada

siri hao mateja wote huku bongo kwao sio haba na waliacha shule za ghali wakenda huko wana asili wa uarabu shombe shombe nguo tu wanazo za kutosha ila saa 7 mchana jua kali unakuta wametinga
Waliendekeza starehe,,,kongole kwa hao waliotusua
 
Wewe exposure yako na diaspora ni failures wawili watatu wa Tangi bovu? You don't know shit. Hata Dubai inawezekana hujafika.
Kwani nikifika Dubai kunaniongezea nini?nitolee unga wako hapa
 
Waliendekeza starehe,,,kongole kwa hao waliotusua
sisi mtaani kwetu machalii wengi wanaenda tatizo bangi wao kupost tu mapicha we acha wanachezea pesa wakirudi huku wako hoi ila wanaojitambua wanafika mbali sana kw kweli
 
sisi mtaani kwetu machalii wengi wanaenda tatizo bangi wao kupost tu mapicha we acha wanachezea pesa wakirudi huku wako hoi ila wanaojitambua wanafika mbali sana kw kweli
Vijana wengi wanashindwa tumia fursa vizuri...
 
Mimi diaspora nilokutana nao kwakweli wanavutia kila idara,yaani unatamani huyu angekuwa mme wako.

Yaani hao wawili nilokutana nao wacha wee sijui magari ya maana ni wao, sijui nyumba nzuri, ni wao, kwakweli siwezi wataja hapa ila mlipo silute kwenu.

Diaspora nyote ntaoaga mbinguni huku duniani hakuna wake zenu.

TATIZO WALILO NALO..........NI KUOA

diaspora popote mlipo aliyewaroga dawa aliwawekea mapenzini ili msioe. Poleni sana.
 
Mwenzio kakutana na watatu vimeo kahukumu jamii nzima!
 
Mimi diaspora nilokutana nao kwakweli wanavutia kila idara,yaani unatamani huyu angekuwa mme wako.

Yaani hao wawili nilokutana nao wacha wee sijui magari ya maana ni wao, sijui nyumba nzuri, ni wao, kwakweli siwezi wataja hapa ila mlipo silute kwenu.

Diaspora nyote ntaoaga mbinguni huku duniani hakuna wake zenu.

TATIZO WALILO NALO..........NI KUOA

diaspora popote mlipo aliyewaroga dawa aliwawekea mapenzini ili msioe. Poleni sana.
Natamani nikufanye Nkumbu wa South [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom