dada haya ni matokeo ya watu kugeuza mahusiano ya kimapenzi kuwa anasa badala ya upendo halisi. kweli haiiingii akilini kuwa umpendaye kwa dhati akuume zaidi anapokuacha (japo yu hai) kuliko anapokufa! kumbuka kuachwa ni tukio moja lakini kufa ni mawili ndani ya moja (two in one) yaani ni kuachwa na kufa. dada katerero na wengine naomba rejeeni habari ya mama wa kweli mwenye huruma na upendo wa kweli kwa mwanaye jinsi alivyokuwa tayari mwanaye achukuliwe na mwanamke mwingine (asiye mama yake) ili tu mtoto asiuawe! japo alikuwa mwanamke kahaba tu, lakini kwake ilikuwa heri mtoto wake abaki hai mikonon mwa mwanake asiye mama yake kuliko awe marehemu (afe) mikononi mwake! how wonderful is this love! Mungu ni mwaminifu, alitenda hukumu ya haki na hatimaye mfalme ajkajua hakika kuwa huyu ndiye mama halisi wa mtoto. habari hiyo inapatikana katika 1 wafalme 3:16-27, na nimeieleza hapa ili tuone thamani ya uhai wa mtu na tutafakatri maana halisi ya mapenzi, hahusiano na urafiki.