Jaluo_Nyeupe
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 2,824
- 2,264
Duh! Inaonekana una wivu kiasi ambacho upo tayari hata kuua kuliko kuachwa.<b>Mi nikiwa naye huwa naomba yote hayo yasinitokee,ila ikitokea akanipiga kibuti ndio huwa naona bora afe tu,na wakati mwingine namuombea hata akutane na nyoka nikiwepo ili mimi nimsaidie nyoka amng`ate vizuri.</b>
Mkuu umepiga vibuti vingapi na wewe umepiga vingapi! hebu wote hao wageuze marehemu. inakaaje hii
Duh kuna watu kweli wanafikira za kiselfish sijaona mfano.
Yaani yaani unatafuta wepesi wa nafsi yako kiasi cha kujiuliza kama ni bora kwa mwenzi wako kufa kuliko kukuacha.
Huyu alokuwa mpenzi wako unaesema unampenda sana unaweza kumfikiria kufa kweli!
msiba msiba jamani inauma bora kuachana maana kunasiku mtakutana na kukumbushiana
Yaani umuombee mtu mliyependana afe kuliko kukupiga kibuti mhhhhhhh! Miye hili haliniingii akilini hata kidogo na hata siku moja siwezi kukaa chini na kuomba kitu potofu kama hiki.
Mi nikiwa naye huwa naomba yote hayo yasinitokee,ila ikitokea akanipiga kibuti ndio huwa naona bora afe tu,na wakati mwingine namuombea hata akutane na nyoka nikiwepo ili mimi nimsaidie nyoka amng`ate vizuri.
Hivi kuna aliyeombea mpenzi wake afe? Naona watu wengi hapa wamekosea kulisoma swali/ kusoma kichwa cha mada!
Mimi nilivyoelewa ni kwamba matukio yote mawili, kupigwa kibuti na kufiwa na mpenzi wako yote yanauma. Mwanzisha mada anataka kupata maoni ya watu kuhusu maumivu yepi ni zaidi. Ni hivyo tu labda yeye mwanzisha mada aje aseme tofauti.
Sijasema kwa kuwa ameniacha basi bora afe, ila nilitaka kujua tofauti ya maumivu yatokanayo na matukio yote hayo mawili, nadhani waliowahi kufiwa na kuachwa wangeweza kutuhabarisha zaidi,
dada haya ni matokeo ya watu kugeuza mahusiano ya kimapenzi kuwa anasa badala ya upendo halisi. kweli haiiingii akilini kuwa umpendaye kwa dhati akuume zaidi anapokuacha (japo yu hai) kuliko anapokufa! kumbuka kuachwa ni tukio moja lakini kufa ni mawili ndani ya moja (two in one) yaani ni kuachwa na kufa. dada katerero na wengine naomba rejeeni habari ya mama wa kweli mwenye huruma na upendo wa kweli kwa mwanaye jinsi alivyokuwa tayari mwanaye achukuliwe na mwanamke mwingine (asiye mama yake) ili tu mtoto asiuawe! japo alikuwa mwanamke kahaba tu, lakini kwake ilikuwa heri mtoto wake abaki hai mikonon mwa mwanake asiye mama yake kuliko awe marehemu (afe) mikononi mwake! how wonderful is this love! Mungu ni mwaminifu, alitenda hukumu ya haki na hatimaye mfalme ajkajua hakika kuwa huyu ndiye mama halisi wa mtoto. habari hiyo inapatikana katika 1 wafalme 3:16-27, na nimeieleza hapa ili tuone thamani ya uhai wa mtu na tutafakatri maana halisi ya mapenzi, hahusiano na urafiki.
Miss umeongea vyema, sasa tupe uzoefu wako ulivyoachwa na mpenzi uliempenda kwa dhati au ulipofiwa na mpenzi uliempenda kwa dhati, kipi kilikuuma sana, ulichukua mda gani kumsahau huyo mtu