Wana JF nimekuwa nikijiuliza siku nyingi swali hili na sipati jibu sahihi.Utakuta umempenda mtu unaona ni heri umueleze kilicho moyoni mwako tena kwa upendo na upole tu,lakini matokeo yake majibu utakayokutana nayo inakuwa kama vile ni adhabu,utaambiwa huna adabu,kamtongoze mama yako,utapewa misonyo,pengine hata kichapo toka kwa watu,wengine waliwahi hata kusakiziwa mbwa,na mbaya zaidi unawezakuta mtu hakutaki lakini anaamua tu kukukomesha kwa kukupa shida zake zoote na wewe kwa kuwa umependa basi utamtimizia na bado unaambulia patupu.Mengine tunayokutana nayo wakuu mnaweza kuongezea lakini swali langu ni hilo,je kutongoza ni kosa mpaka wanaume tustahili adhabu zote hizi?
Blaza tatizo kubwa ni timimg.
Kila kitu duniani ni timing tu.
ukisoma alama za nyakati unaweza mpata yeyote umtakaye.
Uhandsome pekee si hoja Shule mmmh!
Pesa, nayo wakati fulani haioni ndani.
Timing ndo kila kitu blaza.
ukitongoza onyesha kwamba umezimika, siyo kwa masafa mafupi bali ya kati.
Eti maneno mawili matatu mara unaonyesha nia na dhamira ya kula uroda.
Wakati mwingine mimacho yako au hata posing yako inaonyesha jinsi unavyotamani.
Mademu wengi cha kwanza wakipendacho ni mahusiano, ni urafiki siyo majambos.
Majambozos ni matokeo tu.
Mimi pamoja na shati langu la kutoboka mabega, enzi zangu nisha wahi tembelea mijiwanja ya nguvu bila nini wala ni.
Blaza timing blaza.
Usisukumwe na hamu ya kutaka uroda, ujenzi wa hoja na mfuatano wa mambo ndiyo jambo la kujenga msukumo.
Usilazimishe mambo hata siku moja.
Ukiwa huku majuu pochi ndo inatongoza.
Huku hapendwi mtu kwanja lake wala sura,inapendwa pochi tu.