Hivi kuwa askari polisi ni tiketi ya kudhulumu raia wema?

Hivi kuwa askari polisi ni tiketi ya kudhulumu raia wema?

Mzee wa old school

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
873
Reaction score
1,405
Habari RAIA wema wa Tanzania, nimekaa nalo sana moyoni, lakini kila kukicha mambo yanazidi kuwa mabaya kutokana na matendo mabaya ya askari polisi.

Siku Mona nilikuwa nimesimama dukani nanunua vocha ghafla defender ya polisi ikaja ikawa inabeba watu hovyo. Kufika kwangu nikagoma nikauliza nimefanyaje? Polisi afu vijana hawaelewi wamekazana kusema kamata Hugo bebaa! Tukabishana sana ndio akaja polisi mwengine MTU mzima kidogo akaniangalia huku kashika bunduki akasema mwacheni dogo. Ikawa pona yangu. Na kipindi hicho nilikuwa mkoa mflani nasoma chuo

Baada ya kumaliza, Mungu mwema nilipata kazi katika taasisi Fulani ya Serikali mkoa fulani, kwakuwa kuna wakati nakuwa mtaani najamii katika kutekeleza majukumu ya kazi. Siku moja nilokuwa mtaani natekeleza majukumu yangu.. Sasa baada ya kumaliza nikawa naelekea kwenye gari ilipo paki niondoke.

Nimesimama nashangaa polisi wamevamia wamewashika vijana nilikuwa nao tumesimama nashangaa wakanifuata na Mimi na begi langu eti wananiambia pigs chini, nawauliza nimefanyaje jibu lao tulia wewe mwizi. Nikasema dash! Nikaangilia chini nikanyanyua macho nikawaangaliwa, mmoja kakazana shati.

Mwingine akana ninvyo waangalia akaona aibu akasimama mbali. Nikaona niwatolee kitambulisho walivyokiona wakanitoa haraka pembeni wakiambia nenda. Nikauliza hamjaona kama mmenidhalilisha? Hakujibu.. Nikasema sawa ila dunia itawafundisha na Mungu yupo.. Nikaondoka..

Haya ni baadhi tu ya madhirs yalonikuta
Naongea kwenu askari polisi mtatoa hesabu ya matendo yenu siku ya mwisho (nasema kwa imani yangu na ninauhakika na hilo)

Pia ninyi mmetoka kwenye jamiii pia mtarudi kwenye jamii maana hakuna kazi ya kudumi.

Pia dhulma mnayo Fanya laima mtailipa kwa namna yeyote ile maana ndiyo kanumi ya Kimungu na haijawahi kukosea na haitotokea...
 
Kuna baadhi ya askari wajinga wakishika bunduki wanaona washamaliza maisha yote. Kuna wakati nikipita kwenye zile kota zao wanazoishi na mambo yao wanayofanya naishia kisema acha maisha yaendelee. Huwezi kuwa unaliza watu kila siku na Mungu akakuacha.

Ukiangalia maisha ya wanajeshi madhalani JWTZ utaona ni mbigu na ardhi. Mwanajeshi akipita anaheshimika, watu wanmpisha njia na salamu za bashasha. Lakini hawa kina ziro wakipita watu wanatamani warushe mawe na kuwaweke miba njiani. Wamejijengea taswira ya hovyo kabisa mitaani kwa kitumiwa na wanasiasa.
 
Kuna baadhi ya askari wajinga wakishika bunduki wanaona washamaliza maisha yote. Kuna wakati nikipita kwenye zile kota zao wanazoishi na mambo yao wanayofanya naishia kisema acha maisha yaendelee. Huwezi kuwa unaliza watu kila siku na Mungu akakuacha...
Wamesahau kuwa wao no watu kama watuwengine, na watahukumiwa na Mungu kama binadamu wengine
 
Police Tanzakiza

JamiiForums-289452902.jpg
 
Juzi wamepigana risasi huku Tena kwenye TAASISI ya kifedha wamepigana ndani kwny vichumba vyao vya kiulinzi wakaona haitoshi wakatoka nje mmoja akaona ngoja arahisishe kazi akamchapa mwenzake kihamza Hamza kwenye Benki ya CRDB
 
Yelewiiii
 
Hivi hawa watu wakistaafu huwa wanaenda wapi.
Maana kitaa hatuonani.
Au huwa wanahama mitaa.
Wapo wamejaa tele wanaendelea na maisha yao. Wataenda wapi km siyo mtaani baada ya kustaafu
Na wengine wengi bado wapo kazini na unaishi nao hapo mtaani kwako
Si kila polisi ni dhulumati.
 
Kuna baadhi ya askari wajinga wakishika bunduki wanaona washamaliza maisha yote. Kuna wakati nikipita kwenye zile kota zao wanazoishi na mambo yao wanayofanya naishia kisema acha maisha yaendelee. Huwezi kuwa unaliza watu kila siku na Mungu akakuacha...
Wewe ndiyo una akili km hizo lkn kwa taarifa yako ulichosema hapa ni uongo kabisa
 
Hivi inakuwaje mpaka mtu anakuwa polisi? Iyo kazi imejaa laana na uzulumati.
 
Juzi wamepigana risasi huku Tena kwenye TAASISI ya kifedha wamepigana ndani kwny vichumba vyao vya kiulinzi wakaona haitoshi wakatoka nje mmoja akaona ngoja arahisishe kazi akamchapa mwenzake kihamza Hamza kwenye Benki ya CRDB
Hiyo siyo issue hata raia wa kawaida hulambana risasi
Polisi nao ni binadamu km wewe tu
 
Back
Top Bottom