Hivi kuwa single mama ni ulemavu au kosa?

Hivi kuwa single mama ni ulemavu au kosa?

Raynavero

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
38,378
Reaction score
56,047
Habari zenu, sihitaji kashfa wala matusi hapa maana kuna watakatifu humu koo zao hazina singo mama wala walioachana..

Jf wanapita watu wengi mnoo!!! waliojiunga na wasiojiunga naomba kuuliza hivi singo mama siku hizi imekua ulemavu, kosa, dhambi au fursa!

Mimi sielewi maana naona Mara makongamano ya masingo maza, Mara sijui tamasha La singo mama, uwaunge mkono sijui uwachangie...jamani

Hivi wanawake kwa nini tunapenda kujiona sisi ni waathirika wa kila jambo ambalo jamii inaliangali ktk mrengo tofauti...?

Mbona hakuna hayo mambo kwa wababa wanaolea watoto wenyewe?au wao hawakutani na changamoto za kimalezi?

Mimi binafsi sipendi na nachukia hii kitu (mniwie radhi kwa nitakaowakwaza)ila naona kama vile kujidhalilisha flani hivi...au ndo kutojiamini kama tunaweza!kwa staili hii tunataka usawa na wanaume...haitokaa itokee mpk Yesu arudi...!!!

Kama uliweza kubeba mimba,ikataliwe isikataliwe ukajifungua watoto au mtoto wako mwenyewe kwa nini usikomae mbona vijijini huko watu wanatelekezwa na wanalea watoto wao bila misaada?

Kama umetengana na mmeo au mmeachana kama unahisi huwezi kuwahudumia watoto si uwapeleke kwa baba yao?kama hutaki kaa nao Leo mwenyewe!!!

Yaani sasa hivi huku mijini masingo mama naona wanafanywa mitaji na watu wachache kujiingizia kipato na wenyewe wanaona kama wanapendwa kumbe hawajui ukiona umeitiwa fursa basi jua wewe ndo fursa yenyewe!!!

Wapo wanawake wengi wanalea watoto wao tena kwa shida na hawapigi kelele kimya kimya mpk wanakua!

Wamama wenzangu hii mitandao isifanye tujidhalilishe jamani...hebu tupambane kivingine sio mpk matangazo..maana huko kwenye mitandao siku hizi sijui wameonelea biashara ya Kuwakusanya singo mamaz inalipa kila mtu anaibuka na hoja zake!!

Tuinuke tupambane tusipende kujiweka nyuma!!!
 
hili linasababishwa na mitazamo ya kijamii, katika makabila mwngi Tanzania unapozaa ukiwa nyumbani kwenu huonekana kama mkosi, hutengwa, kusemwa vibaya au hata kutoolewa tena.

Kuna jamaii kama wairaqw walikuwa wanawaua mabinti wanaozalia nyumbani.
Wameru kule Arusha pia huwezi kuolewa tena ukizaa ukiwa hujaolewa aubhata ukiachika kuolewa ni ngumu labda uolewe na mzee.

Kutokana na mitazamo ya jamii kila binti anapozaa bila kuolewa au kuachika huathiriwa na hii mitazamo ya jamii inayowazunguka, hili huwaondolewa wengi kujiamini hivyo hujiona hawako sawa na wengine.

Huu ni mtazamo wangu sio lazima niwe sahihi.


Wanaume waliobahatika kuwa na uhusiano au kuoa singo mama wanawasifia kuwa wanajua kupenda, wanajali sana (wanaume changamkieni singo mama mfaidi[emoji12])
 
Kichwa cha habari hakiko sawa. Single ka Ke au Me

Kwa Me
Sababu nyingi.
1. Hajaa tayari kisaikolojia.
2. Hana hela ya kuweza kushi na wife.
3. Mahari bei mbaya
4. Anaona aibu kutongiza
5. Hajui kut.omba
6.
7.
8.
 
Hakuna kitu kama "single mother". Hakuna mtoto asiye na baba.

Kujiita "single mother" ni kujipachika jina la kuhurumiwa. Unacheza na akili za watu.
Sasa kwa nini kutafuta huruma za watu wakati mtu alizaa mwenyewe kwa mapenzi yake...lakini sasa hivi imekua biashara wanatumiwa kutafuta vipato Mara makongamano ili iweje

Kwa nini wasiishi maisha yao!wajitegemee bila kutafuta hizo huruma
Sichezi na akili za watu ila mmeshangaa kuona linaandaliwa tamasha la kusaidia hao wanaowaita single mamaz!!
 
Back
Top Bottom