Hivi kuwapigia kura CCM sio sawa na kulikumbatia na kuliunga mkono genge la wasiojulikana?

Hivi kuwapigia kura CCM sio sawa na kulikumbatia na kuliunga mkono genge la wasiojulikana?

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
38,298
Reaction score
72,863
Genge la "wasiojulikana" limekuwa likitamba tangu mwaka 2016 mpaka hivi tunavyozungumza.

Na waathirika wa genge hilo ni upande mmoja tu wa siasa zetu.

CCM ambao wameshika dola ni kama vile hawataki kuwashughulikia genge la "wasiojulikana."

Katika historia ya ulinzi na usalama ya Tanzania hakuna genge la kihalifu lililodumu muda mrefu kama genge la "wasiojulikana."

Mazingira hayo yananifanya niamini kwamba genge hilo linakingikiwa kifua na watu wazito wanaotoa amri na maelekezo kwa vyombo vya dola.

Swali la kujiuliza ni kwanini hakuna mwana-CCM aliyedhulumiwa na "wasiojulikana?" Hiyo kinga wanaitoa wapi? Je, CCM inahusika na genge hilo?

Majibu binafsi kwa maswali hayo hapo juu, yamenielekeza kuhitimisha kuwa CCM ndio wahusika wa genge la " wasiojulikana. "

Kuipigia kura CCM ni kukubali na kubariki unyama na ukatili wa genge la " wasiojulikana. " Ni kuunga mkono UGAIDI WA KISIASA hapa Tanzania.
 
wasiojulikana kuna kipindi watafikia hata sio mwanasiasa utafikiwa endapo wakiona ufurahishwi na serikali kwa jambo lolote .
Wafanyabiashara mtafikiwa.
Wakulima mtafikiwa.
Wafanyakazi mtafikiwa.
Wavuvi na wafugaji mtafikiwa.
Bodaboda mtafikiwa.
Chawa mtafikiwa.
Polisi mtafikiwa.
Lucas mwamshamba utafikiwa tena ukiwa na maparachichi yako yamekosa soko rudewa
 
Wale kwani wanapigiwa kura?

Kama ni kura hupigiwa na wajinga wachache vijijini huko, ccm hutumia udhaifu wa muundo wa tume kuiiba kura na kujitangazia ushindi!

Leo, nenda hata huko vijijini kwa wajinga uwaambie ccm hoye? Wataitikia tu iwapo umewapa rushwa
 
Genge limejigicha ndani ya CCM dhahiri kuwaunga mkopo no KUKUBALI WATEKAJI na wasiojulikana
 
..vyombo vya dola vinavyosimamiwa na CCM vimeshindwa kuwadhibiti wasiojulikana toka mwaka 2016.
 
Ni kwakua tu Tanzania tuna amani ya woga, vinginevyo barabara zingekua zimejaa watu na matairi ya magari Yakima kumdai Mdude.
 
Back
Top Bottom