May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Siku chache zilizopita nilikuwa safarini na nimeona maeneo mengi Wakulima wakiweka mbegu mashambani.
Ingawa sikuweza kujua aina ya mbegu wanazopanda lakini kwa mazoea tuliyonayo wengi wao watakuwa wanapanda mahindi au Maharage.
Ni jambo la kutia moyo kutokana na kusuasua kwa mvua za msimu lakini najiuliza kama wana taarifa sahihi kutoka kwa Mamlaka za hali ya hewa.
Hivi kwa nini Watu wa TMA na Wizara ya Kilimo wasijitokeze wakiwa pamoja na kutoa ushauri wao badala ya kuacha TMA kuongea tu kama kutimiza wajibu na kisha wanakaa pembeni na kuacha mambo yaende yatakavyokuwa?.
Hawa Wakulima wanapanda sasa hivi na tunawaangalia tu alafu wakikosa mavuno tutasema tuliwaambia hamkusikia...ni nani wa kufuatilia kujua kama wana taarifa za TMA na ni nani wa kushauri ni zao gani wapande?.
Au waachwe tu wacheze kamari, wakipata wapate wakikosa wakose?.