Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,986
- 5,058
Kijana wa kiume unapofikia age ya kuoa,mama na kina dada wanaanza kukupa wosia kuhusu mtu wa kuoa. Mbona madingi huwa wanauchuna? Nipo kwenye hiyo age,siku moja nilikuwa nastorika na mama anielekeza kuhusu mke ninayetakiwa kuoa na sifa zote alizotaja ni zile anazopenda yeye. Kuna vitu vngine mi naona kawaida lakini yeye hapendi. Walipokuja dada zangu nao wimbo ukawa ule ule! Mbona dada zetu cc hatuwapangii mume wa kuolewa? Au mbona akina baba huwa hawawapi wosia mabinti kuhusu wanaume watakaowaleta? Mama na dada zangu nipeni ufafanuzi kuna siri gani huwa inawaumiza? Sory kwa wale watakaofikiri ni teenage marriage niko above 26yrz.