UFUNUO WA TANZANIA
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 471
- 166
Jana kikwete ametua dodoma eti kuongeza jitihada Za kufikia maafikiano kura iwe ya Siri au ya wazi. Kama kweli hawa wanasiasa waliouchukua huu mchakato kama ni wao wana utimamu wa akili hadi washindwe kuafikiana kitu kidogo Kama hicho. Wameshindwa hata kusema basi mjumbe ataamua binafsi atumie kura ya wazi au ya siri kwa kadri atakavyoona I nafaa ili tuendelee Mbele. Kama wanashindwa kuafikiana kwa hili dogo je makubwa yali hoop Mbele watayaweza? Tangu siku nyingi Kama wasomi tulipinga wabunge na wawakilishi kujigeuza kuwa wajumbe wa bunge hili. Ili pasa waendelee na majukumu Yao na wachuguliwe wananchi wengine kwenda Kufanya hiyo kazi na wasiteuliwe na raisi. Kwa mwenendo huu hatupati katiba mpya na dhamira ya rais kuwa mchakato ukivunjika tutaendelea na katiba iliyopo itafikiwa.