Hivi kwa Watu wenye akili timamu kura ya Siri au ya wazi imlete Kikwete Dodoma kuamua

Hivi kwa Watu wenye akili timamu kura ya Siri au ya wazi imlete Kikwete Dodoma kuamua

UFUNUO WA TANZANIA

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
471
Reaction score
166
Jana kikwete ametua dodoma eti kuongeza jitihada Za kufikia maafikiano kura iwe ya Siri au ya wazi. Kama kweli hawa wanasiasa waliouchukua huu mchakato kama ni wao wana utimamu wa akili hadi washindwe kuafikiana kitu kidogo Kama hicho. Wameshindwa hata kusema basi mjumbe ataamua binafsi atumie kura ya wazi au ya siri kwa kadri atakavyoona I nafaa ili tuendelee Mbele. Kama wanashindwa kuafikiana kwa hili dogo je makubwa yali hoop Mbele watayaweza? Tangu siku nyingi Kama wasomi tulipinga wabunge na wawakilishi kujigeuza kuwa wajumbe wa bunge hili. Ili pasa waendelee na majukumu Yao na wachuguliwe wananchi wengine kwenda Kufanya hiyo kazi na wasiteuliwe na raisi. Kwa mwenendo huu hatupati katiba mpya na dhamira ya rais kuwa mchakato ukivunjika tutaendelea na katiba iliyopo itafikiwa.
 
Huyo ndo rais tulie nae..! Hivi waziri mkuu kazi yake nini?

Hii nchi ni bora tungekuwa hatuna rais kabisaa... Kuliko huyu ------.
 
Ndugu yangu UFUNUO WA TANZANIA; Huo ndo ukweli wa mchakato mzima hadi ulipofikia haujachukua maoni ya watanzania na kuayazingatia.Mara zote maoni ya wananchi ya mepuuzwa na uwingi wa CCM hata hatua za Awali niyeye pekee ambaye amekuwa akiingilia kunusuru.

Nadhani kuna ka-ujanjaujanja kanafanywa hapa na CCM ambako baada ya tamko lake tutaanza kuona uelekeo Kamili wa mchezo mzima.BY THE WAY HILI NI BUNGE LAKE AMELICHAGUA YEYE KWAHIYO ANAWEZA KULIAMURU LIFUATE JAMBO FULANI NA LIKAFUATA TU HATAKUWEPO WA KUBISHA UKIZINGATIA MKUU KESHA SEMA "UNYONGE SASA BASI"
 
Tunataka kura ya wazi ili wapinga & wakataa muungano wetu tuwajue kwa sura, tunataka kukomeasha unafiki wa baadhi ya watu -mchana wanavaa ngozi ya kondoo lakini usiku ngozi ya chui - hatutakubali kabisa.
 
Uzembe wa waziri mkuu vitu vidogo anataka rais ndo ashughulikie yeye rais,pinda, wabunge wamchaguliwa kwa kura ya siri leo wanikana?
 
Back
Top Bottom