Kuna kitu hakiko sawa nahisi sijui kama wakuu mmeona hicho kitu unajua nimekuwa nikijiuliza sana why hizi academician Positions zimekuwa readvertsised mara nyingi ikabidi nijaribu kudadisi na hili ndio jibu langu japo mnaweza kosoa kama sitakuwa sahihi
Tuanze kuangaza zamani vyuo vilipataje Wakufunzi tuchukulia case study iwe UDSM!! Hapohapo tukumbuke hakuna chuo wala kozi ya kusomea ili uwe mkufunzi!
Zamani wale waliokuwa wanafanya vizuri hasa kwa undergraduate Degree chuo kiliwabakiza wanakuwa Tutorial assistant katika idara yenye uhitaji au alipofanya vizuri anawekwa katika hiyo idara anatafutiwa scholarship kwa urahisi tu anasomeshwa Masters hadi PhD katika vyuo bora kabisa ulimwenguni ukisoma ile Prospectus ya chuo utaona huyu sijui kapta PhD Oxford, huyu, Njimegen yule Alberta huyu sijui Cape town huyu Kwazulu natal yule sijui Calgarly univeristy na seneti ya chuo ndio ilikuwa na mandate ya kuajiri sasa leo
Hii ajira zote zinapitia Utumishi Dadeki kazi ipo hapo!? Hivi kwa ulimwengu wasasa nani asome hadi PhD katika Programmes ambazo hata kupata ajira ni kipengele tu Yaan mtu asome Fine and Performing art sijui libarary studies , Sijui Developments studies Yaan alenge kuwa mkufunzi nani huyo!??
Mfumo wa Utumishi ni mzuri kwa kazi za kawaida tu ila academician naomba wawaachie tu vyuo wenyewe waandae wakufunzi wao!!
Kuna watu nawafamu wamemaliza pale UDSM na GPA 4.4 za MBB sujui Microbiology wapo tu kutaa wanauza asali toka kaliua Tabora wanaleta DODOMA hapa!!
Ukichunguza kwa umakini snaa utagundua zile Programmes zisizo na future na zisipendwa nyingi ndio zinaongoza kuwa READVERTISE sana wakuu
MWISHO