Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rebecca upo wewe???ni utoto tu
Ni wivu tu. Wanadiss huku wana mkubali gizani
Kwa nini unamchukia Alikiba? Kwa kifupi Diamond na Alikiba wanachukiwa sana hilo halina ubishi kama mfano ulioutoa hapo yaani hvyo kwa watanzania hii kitu hauiepukiki kamwe na kuwabadilisha watanzania hii kitu haitakuja kutokeaKiba hana Mashabiki bali ana watu ambao wanamchukia Mondi na sababu kuu tulizoea wasanii wetu ku hit kwa mda fulani na kupotea na kwenda kimataifa tukatambulisha mziki wetu ilikua kama ndoto sasa dogo kaweza ndio tatizo linaanza hapo. Wabongo tunapendwa kunyenyekewa yaani media na mameneja uwahusudu sasa Mondi kabadilisha hili kutoka kwa ma meneja njaa mpaka kuwaajiri yeye kitu ambacho kama kilikuwepo basi hakikua kwa kiwango cha Mondi na kuikuza brand yake mpaka imefika hatua hategemei sana Media kutambulisha kazi zake.
Sasa wa bongo tunapenda tu unafiq na kuonana tukiwa masikini hao kina Kiba kwenye game kitambo wameifanyia nini nchi yetu? Dogo kaweza na atafika mbali tumuunge mkono anaweza.
(samahani kwa povu langu nimeamka nazo)[emoji4] [emoji4] [emoji4]
Watanzania wengi wamekata tamaa ya maisha yao na mond katoboa life ya kibongo,asili ya watu waliokwama ni kuwaombea mabaya waliofanikiwa ni WIVU WA KIJINGA sana.Diamond Platnumz ni mwanadamu ana madhaifu yake kama alivyo binadamu yeyote yule. Lakini katika picha kubwa na kimuziki huyu ndugu yetu anaiwakilisha nchi vyema sana huko nje.
Nadhani hili ndilo la Msingi na tungebaki kuliangalia wote kama Watanzania. Kuwa na timu siyo makosa hata Yanga na Simba ni Wapinzani wakubwa lakini tukija kwenye Taifa Stars hizo timu tunazivua na tunavaa Utaifa. (Huu ndiyo Uzalendo jamani)
Utaifa ukiisha tunarudi kwenye timu zetu na kuanza kung'oa viti pale uwanja wa taifa. Hivyo basi kwenye kujenga sifa za wasanii wetu awe Ali Kiba, Diamond au Vanessa Mdee tushindane humu ndani lakini tusifanye chuki kiasi cha kutaka kuchafua sia zao. Hao ni watoto wetu kabisa,watoto wa nchi hii: Hakuna mzazi anayetup watoto jamani.
Tumtie moyo Alikiba na tumtie Moyo Diamond: Pia tuwakosoe pale wanapofanya vibaya hali tukiwa na dhamira safi kabiaa ya kutaka kuwajenga kimuziki. Tuepukane na fitna,majungu na uzandiki l: haya mambo hayajengi kabisa.