Kuna mambo yanakera sana mkuu. Angalia sasa hivi SSH alivyokwenda kujikuta kakwama matopeni:
1. CCM chawa wa mwendazake hawataki kusikia Corona, chanjo, tahadhari au yatokanayo. Pia hawataki katiba mpya.
2. CCM chawa wa SSH hawataki katiba mpya ila wanamwunga mkono, kwenye msimamo wa Corona na yote yatokanayo.
3. Chadema waliokereka na mwelekeo wa SSH baada ya msimamo wake kuhusiana na katiba mpya kukolezwa vilivyo na sakata la Mwanza na yatokanayo yake yote, hawana mpango naye tena.
4. Wengine waliobakia wakiwamo CUF, ACT, na wasio na vyama na ma liberali wasioeleweka wanataka nini.
#1 ni wengi kuliko #2
#3 ni wengi kuliko #4
#3 wanaweza kuwa sawa na #1 kiidadi.
Kwamba Chadema ni wanyonge? Labda kama mleta mada ana maana kuwa SSH amewavunja moyo na hawana sababu tena ya kumwunga mkono kwa lolote.
Huwafanyii watu ukiukwaji mkubwa wa haki zao, ukatumia polisi kuwakamata, ukawabambikizia kesi nk kisha ukategemea wakuunge mkono.
Katikati ya kuelekea chanjo ya Corona kutoka kwa beberu waliyeaminishwa wapumbavu kuwa ni mchawi wetu mwenye kutupiganisha vita vya kiuchumi, chanjo kwetu ni muhimu zaidi kwa sasa kuliko mengine yote:
Utu uzima dawa, na ya kale ni dhahabu. Mzee Warioba ni mtu wa kuonwa kwa ushauri (consultation) na wote wenye nia njema na nchi hii na hasa wale walio wazalendo. Hii ni kwa wote tokea serikalini na hata wanaopambania kupatikana katiba mpya. Mzee Warioba yuko wazi kuhusu umuhimu na udharura...
Ifahamike kuwa jukumu la kwanza la serikali yoyote ni kuwaunganisha watu wake na kupata uhalali tokea katika walio wengi.
Serikali inayoshindwa kuwaunganisha watu wake na ikashindwa kupata uungwaji mkono wa wengi hupoteza uhalali wa kuwapo kwake.
Kumwacha SSH akale alikopeleka mboga hakuwezi kuitwa unyonge:
Ni wazi kuwa kwa makamanda wengi suala la chanjo ni muhimu lililokuja likiwa limechelewa mno. Inafahamika kuwa Chanjo hii imetufikia kutokea kwa tulioaminishwa kuwa ndiyo walio wachawi wetu wakuu yaani mabeberu. Ni barakoa, PPEs, sanitizers nk? Vyote vikinasibishwa na upigaji wa mchawi beberu...
Kwetu chanjo inaendelea kuwa ni muhimu na umuhimu wake kwa sasa unaishia kwetu sisi wenyewe. SSH na washirika wake wakale waliko peleka mboga.
Cc:
Erythrocyte Frank Wanjiru Salary Slip Bujibuji Sky Eclat
imhotep Jumbe Brown Mshana Jr