Hivi kwanini hapa Tanzania matajiri au watu waliofanikiwa kimaisha hupenda kutuongopea kuwa wao wanafanya kazi kwa bidii?

Ducinaltum

Senior Member
Joined
Oct 9, 2022
Posts
175
Reaction score
137
Hivi kwanini hapa Tanzania matajiri au watu waliofanikiwa kimaisha hupenda kutuongopea kuwa wao wanafanya kazi kwa bidii?

Kuna mmoja nlimskia anasema yeye hulala masaa matatu tu, hivi huo ni utajiri au mateso?

Elon Musk tajiri namba moja duniani yupo mtandaoni muda wote, na ana hat na watu, ila hizi tajiri za matunguli zinadai zinafanya kazi kwa bidii
 
Hahahaha Daah
 
Huwa huwaelewi vizuri. Wanaposema wanafanya kazi kwa bidii, wanamaanisha kazi halali au haramu.
 
Kwasababu ni kweli, kwa mtazamo wao.

Hata mtu mwenye bahati anajiona ana bidii, kuna vingi amefanya kabla ya hiyo bahati.

Anayepita njia za panya pia hutumia bidii.

Mambo ya uchawi ni ujinga tu mnaopenda kuamini, hamtaki kuona mbali.
 
Hahah, bas kuna utofauti wa matajiri wa kwetu na wengine. Kiukweli mtu hawezi kutoa siri zake za ndani za mafanikio yake, instead atasema vitu cheap cheap tu.

Hawawezi kutuambia siri halisi za mafanikio.
 
Kwa uzoefu wa miaka yangu hapa duniani. Ni kazi ngumu sana kuwa bilionea bila magumashi hapa Tanzania

Unafikiri hata kufoji nyaraka ili mtu apige dili ni kazi rahisi? Ukienda kichwa kichwa unafungwa.

Mtu anaweza kutumia siku kadhaa anakesha ili kufoji nyaraka mana anakuwa anajiuliza maswali kadhaa ili kufuta ushahidi mara pamekucha, kesho yake tena anaendelea kujiuliza, mwisho wa siku ndio anakuwa analala masaa 3 mpaka mchongo ukamilike.

Au mtu halali anafuata au anasubiri magendo usiku wa maneno.

Pesa nyingi inapatikana mazingira tatanishi. Ndio maana askari wa patrol wa usiku wa manane anaweza kukamata magendo ya gharama tofauti na wa mchana, ndio maana wanasema watu hawalali
 
Hahah, bas kuna utofauti wa matajiri wa kwetu na wengine. Kiukweli mtu hawezi kutoa siri zake za ndani za mafanikio yake, instead atasema vitu cheap cheap tu.

Hawawezi kutuambia siri halisi za mafanikio.
kama kweli unataka kufika kule, utajua tu.

ukishakanyaga ngazi moja, utaiona nyingine iliyoko mbele.
 
Umeeleweka vema sana.
 
Ili ujue jambo fulani ni la uongo lazima kuwe na ukweli.

Haya mkuu, tuambie ukweli wa kuwa tajiri ili tuache uongo wa kufanya kazi kwa bidii
 
Ili ujue jambo fulani ni la uongo lazima kuwe na ukweli.

Haya mkuu, tuambie ukweli wa kuwa tajiri ili tuache uongo wa kufanya kazi kwa bidii
Mim nafanya kaz kwa bidii sana tu, ila ndo naishia maisha ya kawaida tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…