Hivi kwanini hatuwawezi Uganda kwenye soka?

Hivi kwanini hatuwawezi Uganda kwenye soka?

Lakini si tumefuzu
Hoja hapa kwa nini tunashindwa kuwafunga...hivi kwa mawazo yako sasa hivi Uganda wakisikia wanacheza na Tanzania wanashtuka ukilinganisha na sisi kusikia tunacheza na Uganda?

Mimi muda wote nilishajenga hofu kuwa tutafungwa tu.

Hata nikawa kama nalalamika kuwa kwa nini kila fainali tunakutana na hawa jamaa?.
 
Uganda huwezi walinganisha kisoka na Tanzania, kule kunauwekezaji mzuri kwa wachezaji tangu utotoni na michezo wanatilia maanani hasa shuleni, njoo kwa wazee wa connection sasa ujingaujinga tu
 
Jiulize pia mchezaji wa Tanzania aliyesababisha faulo iliyowapa uganda kupiga free kick na kupata goli la kwanza ilkua na ulazima wakufanya ile faulo?. Nidhamu mbovu.
Jukumu la mwalimu ni pamoja na kufundisha nidhamu.Pia hii ni dalili ya kuzidiwa mbinu na uwezo kiuchezaji katika mchezo.
 
Ile AFCON nakataa kwakuwa hata match ya kwanza iliyofanyika Uganda hakuna aliyekuwa amefudhu. Kumbuka ile game ya kwanza ilitoka bilabila. Kipindi cha kwanza Waganda walicheza poa but kipindi cha pili Waganda walipotezwa sana na Samatta angeongeza umakini walikuwa wanakufa 2 wale. Match ya pili ilikuwa lazima Uganda afe.
Nadhani tunaoamini kuwa tulifanyiwa wepesi tupo wengi kuliko wanaoamini tofauti.

Au la basi wao hawakutaka kupoteza nguvu kubwa kujiandaa kwa jambo ambalo walishakamilisha.

Ila bado ni kama ninahisi siasa iliiingia kidogo....hata leo nikisikia tunacheza na Uganda matumaini ya ushindi yanakuwa chini sana ukilinganisha na Jirani wengine kama Kenya, Sudan, Ethiopia, Burundi, Rwanda n.k....sina haja ya kuwataja Somalia, Elitria au Djibuti.
 
Bongo siasa nyingi sana yan hata kuchaguliwa hizi team za taifa ni siasa tu,hawaangalii vipaji wala nni ukweli ni kwamba kuna wachezaji wengi ktaaa wanavpaji katika soccer bt njia ya kufika huko juu ndo wamekaa hawa wapga madili.
Good point
 
Tutaacha kujidharau hadi lini mechi ya kwanza tulicheza kwao(ugenini) tukatoka suluhu, walishindwa kutufunga. Tukacheza nao Taifa tukawaburuza goli nzuri tu, Utasemaje tulisaidiwa?! Kwanini walishindwa kujisaidia wenyewe mechi ya kwanza?!


Shabiki Maandazi.
 
Back
Top Bottom