Hivi kwanini Insurance Companies hazitoi EFD Risiti?

Kudasai

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2016
Posts
214
Reaction score
254
Hapa ninamaanisha makampuni yanayotoa bima za magari, nyumba, na vitu vingine.
Unapokwenda hitaji huduma zao wanafanya mahesabu na unalipa jumla yote including percent ya kodi (TRA) lakini hupewi ile risiti ya EFD!
Sasa tunajuaje kuwa TRA wanapata kodi yao stahiki?
Nimeshatembelea ofisi za bima zaidi ya mbili na wote wanatoa risiti za kwenye vitabu vyao.
Tunahitaji kila mmoja wetu alipe kodi stahiki kwa maendeleo ya Taifa letu.
Tunaomba TRA mfuatilie hili na kila kampuni la bima liwe na EFD.
Ni hayo tu kwa leo.
Asubuhi njema.
 
Serikali inalazimisha kila mmiliki wa gali alikatie bima nilidhani na yenyewe inafaidika kumbe hawana wanachopata
 
Wanatoa ndugu yangu na kama ulikatia kwa agent inabidi akupe kwanza risiti yake kisha akiyafikisha malipo bima ndio anapewa risiti ya efd anakuletea
 
Serikali inalazimisha kila mmiliki wa gali alikatie bima nilidhani na yenyewe inafaidika kumbe hawana wanachopata
Haizalimishi bali ni kujali wale watakaopata madhara ajali ikitokea ili waweze kupata haki yao... Kiuhalisia hata majengo yanapaswa kuwa na bima
 
Haizalimishi bali ni kujali wale watakaopata madhara ajali ikitokea ili waweze kupata haki yao... Kiuhalisia hata majengo yanapaswa kuwa na bima
Hapo sijaelewa bro unaweza kutembea na gali ambalo halina bima na polisi wasikukamate?
 
Wanatoa ndugu yangu na kama ulikatia kwa agent inabidi akupe kwanza risiti yake kisha akiyafikisha malipo bima ndio anapewa risiti ya efd anakuletea
Sijui kama hili linafanyika....
Na ni wangapi hapa MMU mfano wameshawahi kupewa risiti ya EFD!
Ngoja nifuatilie risiti yangu nione ntapewa jibu gani kwa sababu miezi 3 imeshapita sijaitiwa risiti yangu
 
Hapo sijaelewa bro unaweza kutembea na gali ambalo halina bima na polisi wasikukamate?
Ni ngumu na tayari hiyo imeshakuwa sheria kwenye kanuni za usalama barabarani
 
Sijui kama hili linafanyika....
Na ni wangapi hapa MMU mfano wameshawahi kupewa risiti ya EFD!
Ngoja nifuatilie risiti yangu nione ntapewa jibu gani kwa sababu miezi 3 imeshapita sijaitiwa risiti yangu
Angalia ulikatia kwa agent au kwa bima wenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…