Naamini Yanga ina viongozi weledi tena wasomi kwa hili walirekebishe mapema maana kama hawataki rangi nyekundu basi wasiwe wanatumia kabisa noti ya elfu kumi (10,000) ambayo ina rangi myekundu inayotumiwa na timu ya Simba.
Kuna watu wanalichukulia suala la logo kama kitu kidogo. Kiukweli logo ni utambulisho wa tasisi fulani na kila taasisi inakuwa imechagua rangi kwa sababu maalum. Kwa hiyo unapobadilisha rangi (corporate colour) kwenye logo ya taasisi husika bila ridhaa yao unakuwa haujaitendea haki hiyo taasisi.
Hebu tuweke ushabiki pembeni kwenye mambo ya msingi, hivi kweli siku ambayo Simba watacheza na Yanga uwanja wa taifa na Simba akawa mwenyeji halafu kwenye matangazo akaweka Simba VS Yanga halafu logo ya Yanga ikawa ipo kwenye rangi nyekundu je Yanga watakubali? Je nchi itakalika? Vipi Yanga wakienda Mbeya kucheza na Mbeya City halafu kwenye matangazo Mbeya City wakaiweka logo ya Yanga kwa rangi nyekundu je Yanga watakaa kimya au watakimbilia TFF? Usichopenda kutendewa usimtendee mwingine maana siku akikutendea utaona unaonewa.
Viongozi wa Yanga hili lipo chini ya uwezo wenu limalizeni mara moja maisha yaendelee kwani watu wanawatazama nyinyi na wala hawatizamwa hawa mashabiki wanaoliunga mkono hapa jamvini.