Heshima Mbele
Ni muda sijaanzisha Mada hapa ila kuna jambao ambalo limekuwa likinitatiza kwa muda sasa ila naamini nyie mnaweza kuwa mnajua?
Hivi kwanini Lowassa anautaka Urais? akichaguliwa atalisaidiaje Taifa? Je, Pesa hizi anazotumia kuweka watu wake kwenye Chama tawala atazirudishaje?
Nimeanza kuogopa sana na kama watanzania wakikubali kuzugwa tena 2015 na kuchagua viongozi ambao wana mvuto wa sura, mvuto wa kutawala bila kuangalia rekodi yao ya nyuma taifa litaenda kubaya sana.
Taifa linaoelekea kupata Gesi na Mafuta linahitaji viongozi makini ambao wataweza kulivusha taifa, kutuondoa kwenye lindi la umasikini na kujenga utawala bora.
Mkuu katika hali iliyopo kwa sasa ni wazi kabisa kuwa usalama wa mafisadi hapa Tanzania upo kwenye kushinda urais mwaka 2015, vinginevyo they will have a huge price to pay and if we get a serious candidate they are very likely to end up behind bars.
Ukikumbuka na machungu waliyopata wengine mwaka 2005 wakati CCM mtandao wanafanya harakati za kuingia madarakani, na events zilizotokea nazitakazotokea hadi 2015, kunaweza kukawa na kisasi kikubwa kwa wanamtandao kama mtandao waki-lose.
So far ukianza kuangalia inaonekana ni rahisi sana kuwanunua watu watakaopiga kura kuchagua mgombea urais kwa tiketi ya CCM, kwa kuwa upepo unaelekea huko. Na imani kwamba CCM watashinda urais by default regardless ya mgombea wake ni nani.
Lakini something dramatic can happen and tilt the balance ndani ya CCM, au mazingira ya kucheza foul yakaharibiwa na wakashindwa kuchakachua kura na opposition wakashinda, hapo mtu anaweza kuingia bonge la hasara.
Hata kama atashinda sidhani kama kuna lolote la maana atakalolifanya kubadilisha hali ya Tanzania, kwa kuwa alipokuwa PM hakuna la maana lililofanyika akiwa kama kiongozi wa serikali, isipokuwa matataizo makubwa yalitokea wakati huo.
Watu walimsifu kwa kubana mianya ya wizi wa fedha kwenye halmashauri, wakisahau kwamba alitaka serikali iwe na mapato mengi ya kuilipa Dowans au Richmond(you know what this means).
Ndio maana ana pesa za kutosha kuwaunga mkono watu anaotaka wawe kwenye mkao wa kumpigia kura. Kwa kawaida mtu akiinvest huwa anapata returns na returns zake zinakuwa kubwa zaidi kuliko investment yenyewe, Ni sisi tutakaolipa.
So kwa EL urais ni kufa na kupona.