Tofauti ya Tajiri na Maskini ni namna gani wanatafuta Pesa
Masikini wengi tunakimbizana na pesa
Tunaamka asubuhi kwenda makazini, na jioni tunarudi tukiwa tumechoka
Asubuhi tunaamka tena, na kwenda makazini
Huu mzunguko unaendelea, mpaka utakapo staafu
Ku "staafu" ni lugha ya kiungwana sana.... Kiuhalisia ni namna nyingine ya kukwambia wewe hutufai tena, tumekutumia vya kutosha
Mafao yako haya hapa, nenda ukafe na trauma za kazi, stress na uzee
Wahenga walikua sahihi, mtaji wa maskini ni nguvu zake
Hata kama kazi unayofanya haitumii nguvu moja kwa moja, iwe daktari, mwasibu, mwalimu etc
Kama namna pekee ya wewe kuingiza pesa ni mpaka ufike kituo chako cha kazi, kila siku tano au hata saba za wiki
Wewe ni maskini, na kwa sababu watoto wako watajifunza mengi kutoka kwako, bila shaka watafata hio trend....
Ukifa ghafla, mwanao hawezi kurithi kazi yako
Matajiri wao ni tofauti
Badala ya kukimbizana na pesa, wao wametegesha mashine zinazowatengenezea pesa
Wana miliki assets,
Wana miliki shule unayofundisha,
Bar unayohudumia,
Gari unaloendesha,
Hospitali unayotibu,
Kituo cha TV au Redio unachotangaza etc..
Literally, wewe pia ni sehemu ya kifaa chao cha kazi
Na hata wakifa, watoto zao wananafasi kubwa ya kurithi na kuendeleza assets walizoacha
Hawana haja ya kufika kituo cha kazi, ili kuingiza pesa
Kuna hii nukuu ya Warren Buffet anasema
"Kama ukishindwa kutafuta namna ya kuingiza pesa hata ukiwa umelala, jiandae kufa masikini"
Njia nzuri ya kuelewa point yangu hapo, ni buibui
Buibui hana haja ya kukimbizana na wadudu
Yeye anajikita katika kutengeneza utando tu,
Utando ndio unafanya kazi ya kunasa wadudu kwa ajiri yake, hata akiwa amelala
Hiki ndio Matajiri wanachofanya, wana miradi yao
ila usiwe excited sana, kiasi cha kuacha kazi yako
Ila kumbuka, kutengeneza assets na kuhakikisha kuna watu wanafanya kazi kwa ajiri yako
Masikini hii elimu hatuna, thus why tunabaki masikini