Nilikuwa katika kijiwe flani cha Wasomo wakati tukijadiliana suala la rushwa, kuna hoja ilianzishwa kwamba moja ya jambo ambalo watu wanalichukuliwa poa ni kwamba linaweza kuwa linachan
gia matukio ya rushwa kuendelea kuwa ngumu kudhibitiwa hasa yale makubwa ni mtu anayeshika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kutokuwa na kinga kisheria.
Huwa tunasikia kwamba CAG anapoteuliwa huwa ni ngumu kumuondoa kwenye nafasi yake japo inawezekana, tofauti na Bosi wa TAKUKURU ambaye ushawishi wa wenye nguvu ya fedha unaweza kusababisha aondoke au aondolewe kwenye nafasi hiyo ikiwa tu ataenda kinyume na wenye nguvu ya fedha na Madaraka.
Je, ni kweli kwamba Bosi wa TAKUKURU kutokuwa na kinga ni sawa na kutokuwa na meno ya kung’ata? Ni kweli naye mkeka unapopita kila mara anakuwa na hofu, hivyo chochote anachofanya lazima alinde maslahi ya waliomchagua?
Nimekumbuka Shigongo aliwahi kuzungumza hii hoja, tuweke mezani tuijadili Watanzania wenzangu.
Pia soma - Shigongo aomba Bunge limpe kinga ya Katiba Mkurugenzi wa PCCB