Hivi kwanini Nahreel na Aika hawapati sapoti ya kutosha Bongo ili hali wako na sound ya tofauti kuzidi wasanii wengi wa kwenye A list

Simply wao sio machawa, uliwaona kwenye kilele cha ccm dom? , je umewaona kweny ugawaji wa tuzo tuzo sjui?? Bhas kama huwaon huko huwez waona popote zaid ya nyumban kwao. Sema kikubwa ni kama mziki wao unakufurahisha bhas inatosha maana wapo miyon kwako.
 
Washazeeke mazee yey badala achague video queen mwingine wa 2000 anakuletea bibi wakimachame wa miaka hiyo ya kikoloni nani atakuwa favorite
 
Washazeeke mazee yey badala achague video queen mwingine wa 2000 anakuletea bibi wakimachame wa miaka hiyo ya kikoloni nani atakuwa favorite
Lakini hapo unazungumzia kwenye muktadha wa video mkuu, vipi kuhusu audio🤣🤣
 
Katika audio anafanya vyema pia ila Kuna namna solo lilipoelekea baaz limewaacha sana labda wakubali kufanya mabadiliko
Kwa jinsi unavyomsikiliza na kuskiliza soko la Dunia unaona soko limekuacha duniani au hapa nyumbani?
 
Fact hawa jamaa wanapiga sana shoo za kimataifa afu wakirudi kama siyo wao tembelea kurasa zao ndo utajua
 
Nawakubali Navy Kenzo ila unapata unachostahili sio unachotaka.

Mziki mzuri utapenya tu sio lazima kiki kama wengi wanavyodai. Fally Ipupa anakiki gani? Wakati P-square wanafungua soko la Nigeria walitoka na kiki gani?

NK mziki wanaofanya sio rahisi kupendwa TZ kama typical bongo fleva na kwa soko la dunia tayari lipo saturated na mziki wa aina hiyo. Hakuna maajabu kwa soko la nje.

Nahreel ni ni bonge ya producer; safari na gere za weusi alipiga yeye zina beat la hatari. Chelewa ya kwao wenyewe bonge la wimbo nk.
 
Na mpaka sasa ni hivyo hivyo tu hata huyu s2kizzy analipwa na diamond angalau vizuri wengine wanalipa hela za madafu tu

Sasa joh atalipa milioni anatoa wapi yule? Alitengenezewa midundo mikali akapiga hela sana ila kumlipa producer ndiyo anaona ubahili wakati hiyo ngoma jnamfaidisha maisha yote huku producer anakufa njaa

Bora nahreel kaacha huo ujinga haulipi
 
Maslahi ya chain ya muziki wetu bado inasafari katika baadhi ya mambo mkuu. Lakini angalau kwa sasa ukilinganisha na tulikotoka though katika upande wa audio production nahisi wakati ule wa kina MAJAN na Master Jay walipiga sana pesa ukilinganisha na hiki kipindi cha hapo kati mpaka leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…