Hivi Kwanini Raia Namba Moja Anawachukia Sana Vijana wa Tanzania Bara?

Hivi Kwanini Raia Namba Moja Anawachukia Sana Vijana wa Tanzania Bara?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,309
Reaction score
15,294
Maana katika Press yake aliongea kitu ya kwamba angelikuwa na uwezo angewakusanya Vijana wote wa Tanzania Bara na kwenda kuwatupa nje ya nchi kama vile Iddi amin Dada alivyokuwa akiwatupa watu kwenye ziwa victoria.

Kiashiria kingine ni kwamba Tangu alivyotimiza lengo lake la kupunguza idadi ya vijana (Tanzania Bara) kupitia kuwaua wakiwa maandamanoni, hajawahi kuonyesha huruma hata kwa kijana mmoja wa tanzania bara aliye uawa, zaidi ya hapo amekuwa akiwatupia maneno wafiwa, wamilia, ndugu na jamaa za wale wote walio poteza watu wao.

Kwenye speech yake tena akaongea habari ya kwamba amekwisha jiandaa na vyombo vyake vya ulinzi ili kuwapunguza idadi ya vijana wa tanzania bara kwa njia ya mauaji pale watakapo timiza haki yao ya kuandamana tarehe 9 Disemba.

Kiufupi mimi najiuliza huenda amechagua njia ya utekaji na mauaji ili kupunguza idadi ya vijana wa tanzania bara (asilimia 60 ya population) ili kupunguza upinzani katika kipindi cha uongozi wake na uongozi ujao.
 
Ndivo alivozaliwa roho yakeiko hivo.
 
Back
Top Bottom