Hivi kwanini wanawake hawapendani?

ibesa mau

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2015
Posts
2,109
Reaction score
1,697
Nilikuwa nausikia msemo mmoja kwamba kikwazo kikubwa katika ku- empower women ni wanawake wenyewe. wanawake ndio kikwazo kikubwa katika harakati za kumuinua mwanamke.

Utakuta mwanamke amefungua duka lakini mwanamke kwenda kununua duka la mwanamke mwenzake ndio inakuwa kazi.

Hivi majuzi kuna mama mmoja alikuwa anagombea ubunge tukategemea kwa kuwa wapigakura wengi ni wanawake katika jimbo hilo huyo mama atafanikiwa kwa kuwa alikuwa na sera nzuri za kuwaendeleza wanawake wenzake , lakini kilichompata mama huyo ni aibu hata kuelezea akaanguka vibaya akawa wa mwisho kati ya watu sita.

Dada mmoja aliwahi kunijibu different gender matters , nikashangaa sana .

Hivi ni kitu gani kinachowafanya wanawake mshindwe kupatana.

Anayejua atusaidie kutudadavulia.
 
wanawake kwa nini nyie hampendani
 
Hata mimi nishawah kushangaa sijui ni wivu gn wanawake na watu wote kiujumla huwa unatusumbua
Nadiriki kusema kama kuna pepo basi watakaoionja hawafiki hata milion nane
 
Ndio zao hizo hata sijui kwanini,ila hata wanyama wana tabia kama hiyo,nadhani feminine gender zote wako hivyo ni maumbile tu.
 
Kwa sababu negative forces hazi attract other ila positive na negative zina attract each other
 
Haya ni mambo ya kimaumbile tu. Coz hata ukisema pengine ni wivu, basi unakuta sio kweli: ni maumbile tuuu wadau
 
Divide n Rule, wakipendana hao wanaume itakula kwetu, kama umeoa wanawake wanne na ukaona wanapendana basi ogopa tena kimbia
 
Nyie wanawake kwann mnaoneana wivu wnyw kwa wnyw
 
Nilishaga wahi kuambiwa eti...MBONA KAMA UNA WIVU WA KIKE..Dah nilichukuia sana.
 
Dharau.......kama tulivyomfanya Batilda Buriani kipindi kile.........alijifanya anaonyesha mazereu tukaungana wanawake wote.........kilichotokea mlikiona............
 
we hukusoma physics..!!!

"like poles repel each other while unlike poles attract each other"
 
Wanaume ndio wanapendana? Au upendo upi unaouongelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…