Ndio ukweli huo, nina uhakika asilimia 100% kwamba wewe hapo kama kweli ni mzazi na una kipato cha maana lazima umempeleka mwanao kwenye shule ya English medium, humu utabisha tu ilmradi lakini kiundani mnalifahamu hilo kwamba mliteleza pakubwa sana kwa kukosa kufunzwa kingereza tangu mkiwa wadogo.
Uwezo wa kuongea kingereza ni muhimu sana haswa kwa jamii yenu ambayo mnaagiza nje hadi sindano, hamjabuni chochote wala kutengeneza chochote humo hata pipi. Hivyo mnategemea kuagiza kila kitu, yaani vitu vinakuja vikiwa na maelekezo kwa lugha ya kingereza, angalia hata settings za simu yako hapo ulipo, hata humu JF kila kitu kipo kwenye kingereza, ni sisi tu tunawasiliana kwa kiswahili.
Wakenya tunapenda lugha zetu za asili, tunapenda Kiswahili kinatuwezesha kuwasiliana kitaifa maana ndio lugha yetu ya taifa iliyo kwenye katiba, lakini pia kingereza tumekipa kipao mbele maana ndio lugha ya wajanja duniani, hauwezi ukafaulu kibiashara kama wewe ni mtu wa ze ze ze kama mlivyo huko kwenu, na ndio maana hata viongozi wenu wanaogopa kusafiri na kuongopa eti wanabana matumizi.
Kuongea kingereza kunataka uzoefu, wacha hilo la kuandika andika humu kwa kingereza maana unao uwezo wa kuhariri mara mia moja na kutumia dictionary pembeni kabla kubonyeza kitufe cha submit. Sisi tunakiongea tangu utotoni, mimi hapa nyumani naongea na wanangu kwa kilugha, ghafla tunatumia kiswahili, kisha unatukuta tukiongea kwa kingereza, ila wao shuleni wamejifunza kifaransa, huniacha kapa wakianza kukitumia. Ujanja wa lugha tangu utotoni, na ndio maana makampuni ya Tanzania yamekomalia kuwaajiri Wakenya sio hayo ya ze ze ze.