Hivi kwanini watu sasa wanaogopa kupeana chenchi?

chuma ulete, bt sina imani nayo hii kitu
 
Panahitaji elimu pana hasa vijijini
Wanachana pesa kidogo kisha wanatupa kipande eti kinga ya chuma ulete
Au kutupa pesa chini kisha kuisugua kwa mguu kisha unaokota pia nayo wanaita kinga
Kutemea pesa kabla ya kuchanya nazingine
Kuipaka mkojo kabla kuchanya na nyingine
......
.....
 
Hii nayo kali
 
Siku hizi wameanza tabia ya kuchana pesa
Unaweza kuta hela ni mpya lakini imechanwa eti kuepusha chuma ulete.
Nina jirani yangu hapa ukimwomba chenchi hakupi hata iweje ila cha ajabu yeye hakupi kabisa sijui yupoje
Watu wana imani za ajabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…