Hivi kwanini wauzaji vipuli wa Bongo ni washamba kiasi hiki!?

SNAP J

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
7,106
Reaction score
8,043
Moja kwa moja kwenye mada kama kichwa cha uzi kinavyojieleza,, sijui ndio ushamba au ndio kukosa maarifa ya kibiashara (business strategies"), au ni ulimbukeni!!???

Kusema ukweli nashindwa kuwaelewa kabisa. Yani haiwezekani jiji la Arusha na Dar es salaam nzima nimezunguka kila kona ya kutafuta spare parts ya Honda crod road eti hamna. Wanasema eti mpaka Nairobi au uagize kutoka Japan.

Kwa kifupi gari zote za Honda Spare zake wanadai ni ngumu kupatikana.

Sasa najiuliza fursa zote hizo wanazowaachia wenzao wa Kenya na nje za nje wakibiashara hawaoni kama wanapoteza!??

WAFANYA BIASHARA WA Watanzania MBADILIKE KWA KWELI.

MUACHE TABIA YA KUFANYA BIASHARA KWA MAZOEA.
 
Kwa kweli kuna magari spare zinasumbua mpaka unaichukia gari hata kama ulilipenda mwanzo. Magari eg Land rover (Freelander), Honda hizo nk.

Gari ambazo hupati shida ni Toyota zote, Mitsubish na Nissan . Mengine kama Ranger over mpaka kwa dealer. Na mikoa mingine hakuna dealer Dahh
 
Ukileta spare za magari kama Volvo Honda Benzi Ford chovelarate hapa Tz utaua mtaji watanzania 90% nimasikini wanaendesha magari ya kimasikini toyota, kutoka Japan tena sio Toyota zote ni selective kama ist, specio hiace wish corona corolla nk. Kama wewe ni strategic business man leta hizo spare,
 
Miaka michache nyuma hata Nissan ulikuwa hupati ni mpaka Nairobi

Wahindi kidogo na Saba General wamerahisisha maisha at least
 
Wewe ndiyo mshamba kwenda kununua gari ambazo siyo majority huku kwetu,uliponunua si ulijua ukitaka spare utaifuata kokote?yaani mtu aweke dukani kitu ambacho gari yenyewe ni moja tu ya shemeji yako,halafu alipe kodi za serikali na pango,umeme na wafanyakazi wakati takataka lako haliuziki,stupid.
 
Tena sio mshamba tu ni limbukeni tu,
 
Mkuu fursa ipi sasa unaizungumzia, kama tangu mwezi uanze wewe ndio mteja wa kwanza kuulizia spare ya honda kwanini ajisumbue kuziweka dukani kwake? Yeye fursa kwake ni spare za toyota kwasababu zinauliziwa kila siku.
 

Honda ni NDOA YA KIKRISTO , Mpaka kifo kiwatenganishe.
 

Kama kweli ulienda kuulizia spare za ‘honda croad road’ lazima uzikose tu maana gari hio haijawahi kutengenezwa duniani.
 
Ni kweli. Shida kubwa nyingine ni hata wabongo wengi wananunua magari kwa kuigana ,ndio maana Toyota zimejaa.
 
Hapa napingana na wewe mkuu.. kununua spare adimu haimaanishi kuwa hautakuwa na spare ambazo ni fast moving kama Toyota au Nissan.
 
Pamoja mkuu nitakucheki.
Nicheki tuma VIN number ya hiyo Honda yako nikuangalizie hapa kesho ila uwe mhitaji kweli sio nifate kuuliza kumbe ulikua unataka tuu kujua Kama ipo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…