Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,818
- 5,555
Wadau wa soka naamini mko salama. Mimi nimeshaachana na ushabiki wa soka krk nchi yetu kwa sababu kadhaa ingawa huwa naifuatilia.
Juzi kumeibuka mvutano kati ya timu ya Simba na TFF kuhusiana na mdhamini mwenza GSM ambao TFF waliusaini bila kushirikisha wadau wengine wa NBC Premier League na wala hawakutaka wadau wengine wa ligi wauhoji; what a shame!
Uzi wangu unahusiana na ubabe wa Yanga kutovaa nembo ya mdhamini wa ligi kuu yaani NBC Premier League kwa kuwa nembo ya NBC ina rangi nyekundu! Huu ni ushamba na ubwege! Msimu uliopita wakati ligi kuu ikidhaminiwa na Vodacom, Yanga waligoma kuvaa nembo ya Vodacom kwa sababu tu ina rangi nyekundu na nyeupe kwa kizingizio kuwa katiba yao haitambui rangi nyingine zaidi ya kijani, njano na nyeusi!
Ikumbukwe kuwa nembo ni alama muhimu inayotambulisha kampuni husika na ndio maana huwa zinasajiliwa kwa sheria za kitaifa na kimataifa na kwa jinsi hiyo hakuna kampuni wala mtu anayeweza kutumia nembo iliyosajiliwa bila idhini ya mwenye nembo.
Rangi ni muhimu sana kwenye nembo yoyote na ndio maana hakuna nembo isiyo na rangi. Nembo insposajiliwa kama trademark pamoja na alama nyingine rangi zake pia huhesabiwa kuwa ni sehemu ya nembo. Ndio maana huwezi kukuta Cocacola ina rangi zaidi ya nyekundu, nyeupe au nyeusi. Ukikuta soda ya cocacola imewekwa kwenye kadha au chupa iliyoandikwa cocacola kwa rangi ya bluu na kijani huwezi kuthubutu kuinunua kama cocacola.
Kwa maana hiyo, Yanga, kwa misimu miwili sasa imekuwa ikiingia kwenye mivutano na TFF na wadhamini wa ligi kuu kwa kugomea kuvaa jezi zenye nembo za wadhamini. Huenda hata kujiondoa kwa Vodacom kwenye udhamini wa ligi kuu kumechangiwa na upuuzi huu maana hakuna nembo ya Vodacom yenye rangi nyeusi! Vivyo hivyo, nembo ya NBC haina rangi nyeusi, ile sio nembo ya NBC inayofahamika, kutumia nembo ya NBC ikiwa rangi tofauti na zilizosajiliwa kisheria ni kosa kisheria kwa kuwa nembo rasmi ya NBC haina rangi nyeusi.
Ifike wakati TFF na Wizara husika wakae na vilabu vyote vya ligi kuu na waje na suluhisho la suala hili, ikiwa kila klabu itadai kutotambua nembo ya wadhamini wa ligi kwa wakati husika itakuwaje? Kila klabu ikitaka nembo ya mdhamini ilingane na rangi zao timu zao itakuwaje? Tiache kulea ujinga, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Kama klabu haitaki kutambua nembo ya mdhamini basi isipewe haki ya kupokea chochote kutoka kwa wadhamini.
BTW, nikija kwenye suala la Yanga kugomea rangi za nembo ya mdhamini mbona walishiriki michiano ya CAF champions league na walivaa nembo ya Total ambayo ina rangi nyekundu? NAWASILISHA.
Vv