Hivi kweli kuna watu wanapiga hela online? Mimi naona kama uzushi tu!

Ni kweli ,tatizo ni namna ya kuwapata mkuu,kama unafahamu naomba bas connection
 
Affiliate marketing inakuaje mkuu?
 
Kwa uzoefu wangu online business inayolipa ni zile za aina ya upwork, affiliates na hizi za contents writing, hizo kweli zinalipa ial nyingine siziamini
Safi kabisa, hata clickworker kama ukiweza jiunga, pia youtube uki post video nzuri na watu kuangalia, ila hizo hela zote zunakuja kwa visenti vya dola, kwahiyo watakiwa kuhenyeka kisawasawa upate mshiko wa maana..
 
Affiliate marketing inakuaje mkuu?
Affiliate marketing kwa lugha rahisi ni udalali.

Kuna bidhaa zinazouzwa mtandaoni, kwahiyo wewe unachokifanya unasaidia kutafuta wateja, mtu akinunua kupitia LINK yako wewe unapewa commission ( gawio ).

Bidhaa zinaweza kuwa web hosting, vitabu, maduka ya mtandaoni, software, huduma za kibiashara mtandaoni n.k
 
Ndugu WATANZANIA WENZANGU BIASHARA YA KULAUMU VIONGOZI KILA SIKU HAITATUFIKISHA POPOTE, KAMA KWELI TUNATAKA MABADILIKO CHANYA , START BY BEING THE CHANGE YOU WANT.
 
Baki na ubishi wako watu wanapiga hela..

Huyu anaitwa kileo cheki profiti yake ya leoView attachment 1825753
Screenshot na loss mkuu ...

Mbona unatuaminisha unapigaa hela ...

Hakuna kitu sijui kuhus forex..

Lazima upigwe tu whether you like or not ...


Yaani huwa ndio mlivo ,kupiga picha profit ,huku loss zipo chini ya carpet [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana kaka me nimekuelewa sana, kila mtu anapojaribu kupiga hatua unakutana na vikwazo cha msingi ni kutokukata tamaa! fanya unachoamini kitakutoa maishani.
 
Kipindi cha mwaka 2014 hadi 2015 kikweli ilikuwa kipindi kizuri wakati huo nafanya google adsense hizi $150 hadi $300 zimenivusha sana nilikuwa na blog yangu so kuna trick tulikuwa tunapeana lakini account sometimes zilikuwa zinafungwa, washkaji wengine walikuwa wanafika hadi $1000 kwa mwezi, siku nilipoenda kutoa pesa pale bank ya posta kwa mara ya kwanza kupitia Western Union hapo posta maeneo ya posta Dar sikuamini macho yangu, so online kuna pesa sio uongo lakini yakupasa kuwa makini.
 
Endelea kubisha wakati wapo top freelancers kama hawa wanaondoka na hela nzuri, huyu jamaa ni rafiki yangu nimefahamiana naye na ni daktari ila cheki kazi zake za Upwork, juhudi za miaka zaidi ya mitano, wakuu tuendelee kujifunza mambo mengi tusingoje ajira rasmi

 
Basi mkuu wewe baki na unachaamini!
 
Yaani hizo sio mishe za kusema mtu anaweza kujiajiri huko ,...

Online businesss iko overrated yaan ukifuatilia kiundani ,hakuna lolote ....

Tuendelee kulima tu
yawezekana ni akili yako au elimu uliyonayo hukuwahi kujifunza IT na related courses ata kidogo now dunia inaenda kasi sana kwa wenzetu digital jobs ni ishu sana yaan ni hot cakes kabisa..
kenya kuna mpaka ATM ya BITCOIN huko kwa wenzetu ndio zimejaa kila mahali sasa ukisema cryptocurrency ni scam cjui kama umeongea baada ya kufanya research hiv unaijua YFI ni nn??

watu wameinvest billions of USD kwenye kutengeneza hzo crypto currency alaf mTZ fulan hv unazi underrate .
alaf ukisikia kujiajiri digital kuna uwanja mpana sana mfano:
-Direct jobs kama upwork, freelance, fiverr etc.

- Affiliate jobs (kuuza vitu vya watu na kupata commision) hii weng wanaifanya sana ata kariakoo utofaut ni kuwa ukifanya online unaonekana ni utapeli but ukichukua nguo kwa mking kariakoo na uuze upewe 3000 kwa kila nguo utakayouza kariakoo unaonekan ni sawa... shame!!!

  • Blogging, vlogging etc
  • Dropshipping (hii ni sawa na affiliate tu)
  • kuuza vitu vyako online kama vitabu, nyimbo, vitu vya kushikika kama unavyoona ebay, aliexpress, amazon nk.
  • Forex exchange, Cryptocurrency (buying and holding then selling or trading). Hii inahitaji ujifunze sana ili atleast uweze kuona matunda ata kidogo.
  • Hosting website and domain selling (tech professionals mostly) unakuwa reseller na unaanza biashara kama vle una server yako.

- Create a system ambayo inaweza kutatua matatizo ya watu (creativity inahitajika)

- Utaleli kama kufungua HIYP programs kama hzo D9, pamafunds, smarthela ukiwa mjanja utatoboa kieahisi na unatakiwa uwe na capital kidogo.

NB: Usilinganishe online business na kilimo ndugu, agriculture ni series mpaka uje upate pesa inahitaji uvumilivu na unaweza ukaweka 5M ardhin na ukaikosa yote.. naongea coz nmepitia na bado some amount nawekaga kwenye mpunga ili mrad tu usije ukaanmbiwa unauza madawa ya kulevya ukiulizwa unasema nalima.

HZO Pamafunds and like zinalipa sana tena sana ila ujue muda wa kuingia kuna system niliweka $300 ikiwa una cku 3 tangu ianze ilivyofika miez mi3 uwez amini nilitengeneza kama $ 3000 na capital yang nikavuta nikaacha mwez wa 5 wakafunga so lazma ujue muda wa kuingia na kutoka kama DECI vle na nmejenga kwa pesa za ONLINE so ukiniambia huwez kutoka nitakuona CHIZI kwangu ila kila mmoja abaki na ANACHOKIAMNI
 
Survey gan hii mkuu inalipa $100+ em funguka kdg
Hii survey naipiga kimagendo Mr, ni legal kwa watu wa USA na UK so nikiiweka hapa tukajazana huko tutashtukiwa [emoji847]
Lengo langu la kuweka izo payment proof ilikuwa ni kuwainspire watu wanaojaribu kufanya online deals wasikate tamaa pesa ipoo cha muhim ni kupambana kutafuta michongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…