Hivi kweli maandishi yote kwenye Bibilia yaliandikwa kwanza kwenye nawe na iliwezekana?

Hivi kweli maandishi yote kwenye Bibilia yaliandikwa kwanza kwenye nawe na iliwezekana?

Kwanza unatakiwa uelewe Bibilia ni collection ya vitabu tofauti tofauti sio kitabu kilichoandikwa na mwandishi mmoja hivyo usishangae hayo maandishi ya muandishi mmoja mmoja kutunzwa kwenye ngozi kama ulivyosema.
 
Achana na hadithi zisizo na kichwa wala miguu.

Screenshot_20231226-175328_1.jpg
Biblia na Quran hazina tofauti na hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela
 
Tangu mwanzo,

BIBLIA imetunzwa Kwa msaada wa Roho mtakatifu.

BIBLIA ni Neno la Mungu, yaani logos.

Tangu enzi na enzi, Roho mtakatifu ndiye amekuwa kiongozi wa mitume na manabii wake kuandika na kutunza neno la Mungu Kwa namna mbalimbali.

Utaona baadhi ya vitabu viliandikwa kwenye gombo, vingine Roho mtakatifu kupitia Malaika, atashuka na kumpa ujumbe wa Mungu Kisha ataandika na utunzani anaengineer Mungu mwenyewe.

Mungu hulitunza neno lake ndani ya MIOYO ya watu wake, hiyo ndio njia nzuri zaidi ambayo kamwe haiwezi kupotea hata zichomwe BIBLIA zote na kufutwa mitandaoni.

NB: Mungu ni ROHO, na wote wamwabudio, imewapasa kumwabudu katika Roho na Kweli. Aamin
 
Kiranga Infropreneur Rabbon

min -me nisaidie kuniitia wengine kazini kwetu kuna kazi… 😂😂😂
Ukishakuwa na vitabu viwili vinavyo pingana maelezo vyenyewe kwa vyenyewe,

Huitaji hata 'D' mbili kujua kwamba ni uongo, Hata ukiwa na 'F' inatosha kutambua kwamba vitabu hivyo ni vitabu uchwara, Hekaya za watu tu.

Zilizotungwa kulishana matango pori, kukaririshana uongo na ujinga.
 
Mungu hulitunza neno lake ndani ya MIOYO ya watu wake
Sasa kulikua na haja gani ya kuwa na bible "hard copy" kwanini hayo maelekezo yote Mungu asingeyaandika tu mioyoni mwetu kuondoa hizi tafrani zinazojitokeza sasa?
 
Sasa kulikua na haja gani ya kuwa na bible "hard copy" kwanini hayo maelekezo yote Mungu asingeyaandika tu mioyoni mwetu kuondoa hizi tafrani zinazojitokeza sasa?
Ilipita miaka Fulani duniani, kuwa na kitabu kiitwacho BIBLIA ilikuwa kosa linalostahili kuuwawa.

Sasa pamoja na juhudi hizo ovu, Bado hayupo awezaye kuifuta Imani juu ya Mungu katika Yesu Kristo.
 
Mungu ni noma wengine aliwapa habari hizi kwa ndoto na maona wakaenda kuandija kwenye mawe na wengine akawashushia moja kwa moja kutoka sijui wapi😀
Kuna namna tumepigwa sana😁😁
 
Ukion hivyo jua umeanza kujitambua endelea kujiuliza na ujiulize hili kwa nini israel ukiubiri habari za yesu unafungwa na ufatilie bLack nazareti ni nani halfu ujiulize tena yesu ni mweusi au mweupe hlf tafuta picha ya yesu inayobebwa na papa akiwa anaingia ibadani ni ya mtu mweusi au nn au julize kwa nn rais tramp anatuita the chosen one ni vingii vya kujiuliza
 
Mimi kama Mkristo, moja ya simulizi ni kuwa maandiko katika kitabi cha Bibilia yalianza kwa kuandikwa kwenye ngozi, mawe na mfano ni amrii kumi za Mungu kupitia Nabii Mussa.

Tunaambiwa Mungu alishusha hizo amrita kwa Mussa na baadae zikaandikwa kwenye mawe na ndio hizi tunazisoma katika Bibilia leo hii.

Binafsi nikiangqlia ukubwa wa Bibilia, najiuliza kweli maandishi yote yale yaliweza kuandikwa katika mawe?

Hata tukisema kulikuwa na njia nyingine ya kuandika, maandishi yote ya kwenye Bibilia wailiwezaje kuyaandika?

Je, haiwezekani tunayoyasoma kwenye Bibilia ni story tu za kutungwa na wanadamu ili walau binadamu wawe na hofu ya kufanya maovu kama kuua, kuiba, kuzini, kudhulumu, n..k?

Ya Qruan siyajua ila sidhani kama yana tofauti na ya kwenye Bibilia kwa maana yalivyoandikwa.

Inafikirisha sana!!
Hapana.

Biblia ni mkusanyiko wa mandishi ya waandishi walioishi kati ya Miaka 5000 Hadi 2000 iliyopita.

Biblia ya Leo kwa mara ya kwanza iliandikwa wayahudi na waliotoka uhamishoni Babylon.

Maandiko yote ya Dini ni legends(ngano au Hadithi)
 
Back
Top Bottom