stonecutter
JF-Expert Member
- Jun 12, 2022
- 1,724
- 2,584
Wakuu,
Ni hivi, leo nikiwa nyumbani akaja dada mmoja jirani yetu akiwa anaongea na mtu kwa simu yake.
Baada ya kukata simu akaniambia kwamba amekuwa anaongea na matapeli na wamemwuliza kiwango cha pesa kwenye akauti yake na kwamba kuna mteja ametuma pesa kimakosa kwenye akaunti ya yule dada na anatakiwa azirudishe (maana tapeli amejifanya ni mhudumu wa mtandao husika).
Baada ya muda kidogo, sms iliingia kwenye simu ya yule dada kuthibitisha kuwa pesa zimeingia na kiwango ni kile alichotaja ila anaporudisha abakize elfu kumi ya asante.
Jamaa akapiga simu kumshawishi dada arudishe pesa. Baada ya majibizano ya muda mfupi kati ya tapeli na yule dada nikachukua simu ya yule dada ili kuongea na tapeli.
Nikamwambia "NDUGU, HELA HAITAFUTWI NAMNA HIYO" Jamani baada ya hapo nimetukanwa matusi yote kwa muda mfupi na mhanga mkubwa ni mamangu mzazi ninayempenda sana (inauma sana).
Je, serikali inajua kwamba raia wake tunatukanwa matusi mazito ya mwilini achilia mbali ya nguoni?
Na Je, serikali imeshindwa kuwatia nguvuni wapuuzi hawa?