PreGE2025 Hivi kweli unaweza kupeleka mil 30+ jimboni wakati unajua hushindi hata ukishinda?

PreGE2025 Hivi kweli unaweza kupeleka mil 30+ jimboni wakati unajua hushindi hata ukishinda?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Benson Mramba

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
766
Reaction score
1,884
Ni mjinga tu au kibaraka kwa malengo maalum anayeweza kufanya upumbavu wa namna hiyo.

Unajua utapigwa na polisi, utaibiwa kura, utaharibiwa mikutano yako ya kampeni na wakishindwa vyote hivyo hata ukishinda hawakutangazi na wanaweza kuua hata watu wako wa karibu, halafu ukachome pesa na rasilimali zako nyingine kwenye uchaguzi kisa nini hasa!?

Ni bora hiyo hela ukalimie, ujenge hata room mbili au ukale bata Dubai uje upumzike na familia yako.

No reforms No election kwa kweli.
 
Mi nasikiaga tangu kitambo Sana kwamba: "Tanzania huwa hatupigi Kura ila huwa tunakwenda kumuidhinisha mtu maalumu ambaye tayari alikwisha chaguliwa na watu maalumu kwa malengo maalumu".
Binafsi huwa naamini iko hivyo; huwa hatupigi Kura, tunaidhinisha(ga).
 
Ni kweli

Ndo maana kuna awamu za wakristo na baadae waislamu
 
Hapo sasa...

Yaani askari kada anamwambia mtu hushindi hata kabla kura hazijapigwa.

"Yaani humshindi hata ufanyeje"

Alijuaje hashindi??
 
Back
Top Bottom