Hivi mabasi ya shule yanakuja lini Tanzania aisee wanavyoteseka kama sio kuonywa ningewabeba mpaka leo

Hivi mabasi ya shule yanakuja lini Tanzania aisee wanavyoteseka kama sio kuonywa ningewabeba mpaka leo

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Nilisoma kwa taabu sana

Hasa upande wa usafiri

Nilipofanikiwa usafiri nkaanza kuwabeba wanafunzi ninaokutana nao na wengi waliishia mwenge ama lugalo shuleni

Siku nikampandisha ndugu yangu mmoja anaenda lugalo kikazi

Akaniambia vitu nikashtuka sana sana

Kaka najua una upendo sana na noah yako hii..na mungu anaangalia haja ya moyo wako

Shida hawa wanafunzi ombea wafike salama kila unapowapandisha

Ndugu ikotokea ajali utajuta kuijua dunia

Aisee ilinichujkua wiki moja na ya kuyaelewa

Kwa sasa bawapita nikiumia sana hasa week hii yaan wanateseka sana sana

Mh waziri husika na mawaziri wengine wapenda watoto

Lini mtaleta haya magari ya shule jaman yaan mpaka watoto wanafika shule wanafika lakn wamechoka sana sanaa

Embu mungu awaonyeshe njia kwa hili
 
Mradi wa mabasi ya wanafunzi ulilambwa na mgombea mwenza mmoja miaka ile kweusi tukiwa vijana tunasoma, leo hii tushastaafu, anyway ilinisaidia sana nilikula kiapo moyoni kwamba sintozaa mtoto mpaka nihakikishe nina gari kwa nilivyoexperience yale mateso, na Mungu ni mwema kweli hadi napata mtoto wa kwanza nilikua na Gx81 gari ya kwanza kbs kumiliki nikiwa kinda na wana hawajapata shida ya usafiri tena kama niliyopata mie hadi wamekuwa watu wazima
 
Wazazi nasi tujaribu kuwapeleka watoto shule za karibu, kila kata kwa sasa ina shule zaidi ya tatu za msingi na sekondari.
Zamani sisi tulikuwa tuna enda shule kwa kuvuka mito mabonde milima , mpaka unafika si haba na hapo ni kwa miguu iende irudi mara miaka saba ya msingi na minne sekondari.
 
Endelea kusaidia mkuu ikibidi ila kila wanaponda Muombe Mungu akuepushie na Mitihani ya Barabarani, niamini hadi utaacha mwenyewe Hakuna kitakachotokea..
Ameen mkuu nafikiria hili Mungu anisaidie wikii hii yaan wanateseka nawaza wakifika shule kichwa imechokaje ndio manaa wnegi asbh wanalala vipindi vya mwanzo sio kwa usingizi uchovu
 
huwa namwombaa Mungu kama nikisoma jwa shida basi watoto wangu ama wa wenzangu wasisome kwa matesooo

Ndio manaa vikaon nikisikia mtoto wa mwamba amerydi shule na kamzigo namwandikisha deni bila riba pelekaa mwanaoo shule

Na uzuri huo sitoi cash unasaini nipe acc ya shule naweka kamata resit yakoooo

Nasubiri upendo na uaminifu wako
 
Mwaka 2011 kama sikosei yaliletwa mabasi ya shule kupitia CRDB bank ila mradi ukafa kifo cha Mende.

Sababu za kufa mradi
1.Magari yale yalikua yanajaza wanafunzi kupita kiasi.
2.Kila kituo basi lilisimama na kutumja zaidi ya dk 5 hivyo ilikua unachelewa.
3. Wanafunzi wengi waliokua wanapanda ni shule za kata wengi hawakua wanajielewa kelele matusi nk.
Nikaacha kupanda hizi gari na nakumbuka nilipandaga mara 2 tu , hivyo shida iliyopo kwa miradi mingi ya umma kufa ni kukosa mkkati madhubuti(kukurupuka) pia raia sisi wenyewe hatuna ustaarabu zile bus wanafunzi walikua wanafanya kila aina ya fujo kuchora siti kubandua makava tena makusudi nk

Hivyo hilo jambo ni kama haliwezekani
 
Kama mwendokasi tu mabasi ya mradi wa kibiashara unafeli, hao watoto wa shule wataweza kupewa usafiri
 
Back
Top Bottom