Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Nimekuwa nikisikia habari za mtu kuambiwa na ugonjwa huu akawa anatibiwa ugonjwa kwa muda mrefu halafu baadae inakuja kugundulika hana huo ugonjwa.
Kuna mdada aliwahi kuhojiwa, aliambiwa na kansa akawa anachomwa mionzi kwa muda wa miaka 2 hadi wakataka kumkata ziwa, ila familia ikampeleka India kufika kule akaaambiwa hana cancer wala nini, ana tatizo dogo tu wakampa dawa na wakamwambia baada ya mwezi atakuwa salama. Dada alikuwa ashapitia majanga mengi mpaka kunyonyoka nywele.
Sasa kuna mke wa rafiki yangu, kwa zaidi ya miaka 5 wanamwambia ana vidonda vya tumbo anapewa madawa ya kutibu vidonda vya tumbo, pia alikuwa anaumwa shingo anaambiwa sijui mshipa gani wa fahamu umebinywa na kitu gani, hapo hayo majibu eti yamepatikana baada ya kufanyiwa MRI, kapigwa X-rays za kutosha pia. Lakini uwa anapata afadhali na hali inajirudia.
Juzi kaumwa sana wakamfanyia kipimo cha endoscope hospital nyingine, kile kipimo cha kudumbukiza camera mpaka huko kwenye utumbo. Yani hana cha vidonda vya tumbo wala nini bali ana fungus kwenye utumbo eti. Pia maumvu ya shingo wakagundua siyo mshipa kugandamizwa bali ana tatizo ingine tu siyo serious kama alivyokuwa ameambiwa.
Nikakumbuka kuna jamaa Mwarabu nilikuwa nasoma naye, mama yake alijifungua mtoto anajicho kama lina weusi, eti hospital ya mkoa wakasema ana kansa walitoe, mama akaamua kumpeleka Nairobi, wakagundua hana cancer yani ndivyo lilivyo tu wala halina tatizo na baada ya muda ule weusi ulikuwa unapotea taratibu mpaka ukaisha.
Sasa nikabaki ninajiuliza, hivi hawa wataalam wetu uwa wanashindwa tasiri vipimo wanavochukua wanafanya kubahatisha tu?