Hivi Madaktari wetu huwa wanashindwa kutafsiri matokeo ya vipimo?

Yaani acha tu, umeandika kama umewahi kupitia hii misukosuko

Kuna kipind kidogo nimpoteze mana kwa huu ujinga
 
Wacha nifatilie huu uzi kuna ntakachoambulia

Ma dk wa tz kuna mahali wanafail
 
Ungetoa na mfano wa hospitali tujue ukubwa wake..

Maana kuna vihospitali vya mitaani tabibu(Clinical Officer) anaachwa kama ndo final say huku elimu yake ikiwa ndogo,na watu huwa wanawaita ni madaktari..matatizo kama haya lazima yatokee..

Note:I don't mean to offend those clinical officers
 
Msi-generalize jamani. Not all. Kuna madaktari wanabaka fani. Mf mtu hajasomea Radiolojia Ila anajifanya kutafasiri Sono au picha za MRI, tegemea anguko na ramri za kipuuzi.

Dr hajasomea Pharmacy vzr Ila anajifanya anajua dawa zote duniani. Medical field is too wide, let us accept our niches where we are expert at!
 
Narudia tena acha kutetea upumbavu.
 

Good answer.
 
Upo sawa sawa nishapigwa wrong treatments mara nyingi sana nikaja kugundua ninachoumwa google huko, hapo nishapigwa pesa almost miezi 9 halafu siponi.
 
Dah. Yani kuna shida kubwa sana kwenye idara ya afya. Dada yangu alikua akilalamika sana maumivu ya tumbo..

Nikamshauri aende kwenye vipimo
vya ultrasound, sasa alivyoenda kwa maelezo yake , yule aliyekuwa anamchukua video alimchukua muda mrefu sana akawa anasema mbona kila kitu kipo sawa.

Sasa kwenda kwa daktari, anamwambia eti umeonekana una maji kwenye kizazi inabidi ulipie dawa za 70,000 ukatumie.

Sasa alivyoniletea taarifa mimi nikashangaa, inakuaje mchukua video asione kitu halafu doctor aseme una maji kwenye kizazi.

Mwisho wa siku, tuliongea na dr mwingine akamshauri sister aache kutumia vidonge vya majira. Mpaka leo miaka 3 sister hajawahi kulalamika tena. Kumbe yule Dr alitaka kutulia 70,000 zetu.
 
Upo sawa sawa nishapigwa wrong treatments mara nyingi sana nikaja kugundua ninachoumwa google huko, hapo nishapigwa pesa almost miezi 9 halafu siponi.
Hata mimi siku hizi uwa nikipata tatizo ninaanzia google au hata nikienda hospital nikiambiwa kitu narudi pia google kujisomea
 
Duh ni hatari kwakweli
 
Kuna jamaa aliwahi kuugua na kutafuta suluhisho zaidi ya hospitali 10.alinzia hospitali kubwa kushuka chini

1.Kila hospitali haikubali vipimo vya hospitali nyingine ulioanzia lazima wakupime upya na majibu yanakuwa tofauti

2.Alikuja kupata suluhisho kwenye hospitali mdogo kabisa

3.Unashauriwa uwe unacheki afya yako mara kwa mara lakini ukienda hospitali ukakuta foleni ya wagonjwa na matatizo makubwa walionao utapanga foleni wewe mzima kweli?
 
Usomaji wetu ni shida eti unapewa picha ya tatizo hata haina muonekano mzuri afu unaambiwa huyo sijui ni parasite gani wakati picha inaonesha ukungu tu,mwisho wa siku tunaishia kukariri
Umeongea Cha maana Sana, elimu yetu ni ya kukariri hata waliotufundisha walikaririshwa
 
Kuna jamaa tumekua nae mtaani babake alikuwa anamiliki duka la madawa,basi yuke mzee akawa anatamani mwanae aje kuwa daktari ingawa mwanae ni kilaza na masomo ya sayansi yalikuwa hayapandi.

Jamaa akawa ana shughuli ya kurisiti ili aendane na ndoto za mzee wake.

Mwishowe jamaa nasikia alifanikiwa kuwa daktari kwa njia walizozijua wao.

Nawasalimu wagonjwa wote wanaoendelea kukutana na daktari huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…