Hivi Madaraka Nyerere ameona kitu cha kulindwa ni jina la Mwalimu Nyerere, na si falsafa zake?

Hivi Madaraka Nyerere ameona kitu cha kulindwa ni jina la Mwalimu Nyerere, na si falsafa zake?

Hujui chochote kuhusu brand, wewe utaona kama jina tu, fatilia brand za majina kama Azam, KFC, Wasafi etc utajifunza mengi.

Jaribu leo kujiita Chiembe Azam kama watakuacha salama.
Tofautisha Brand ya nyota wa mwana mchezo flani,au mfanyabiashara ,na Brand ya Mwanasiasa, Brand ya politician mara nyingi ni free to public!!
 
kufanana jina na kujiita jina sawa ni vitu tofauti.
ningezaliwa naitwa mkorinto Yesu hakuna mtu angenisumbua,ila kuamua kujiita Yesu halafu naamua kuwa muuza mwili sitaachwa salama.
Kwani huyo Steve Nyerere kaenda mahakamani na kuwomba uhalali wa kisheria wa kuwa mtoto wa Baba wa Taifa just kupitia jina tu la Steve Nyerere!!?? Kama kama kafanya hivyo Madaraka aache maneno mengi,yeye aende huko Mahakamani akaweke pingamizi lake na atapata msaada wa kisheria kwenye jambo lake!!
 
Hizo ni personal attacks, unakuwa kama dadako Tulia kueleza mambo kibao ambayo ki msingi hayatusaidii kwa sasa.
Jikite kwenye hoja ya msingi, ulevi wa mtoto wa Mwalimu na kupromote kwake ngumi kunakujaje hapa?
 
unaanzaje kulinda falsafa ikiwa utaacha jina kubwa hivyo litumike na mtu kama steve???

kuchekea watu wapuuzi nawewe unakuwa sehemu yao.
Uwezo wa mtoa mada hapo juu hakika ni mdogo sana. Na inadhihirisha kuwa mtoa mada ni mbumbumbu na hana uelewa au ni mzito kuelewana mada.Au ni chawa kama machawa wengine.

Alichoongea Madaraka ni kuonyesha , kuwa kwa kuwa Nyerere alikuwa mtu muhimu na mwenye uwezo mkubwa sana. Basi jina lake lisitumiwe hovyo na watu ambao hawana sifa kama yeye. Mfano Steven hana sifa yeyote ya kisiasa au ya kusimama na kama mwanafarisafa kupambana na kutoa hoja nzito nzito duniani kama Nyerere.

Kwann anaitwa Nyerere. Wakati ana sifa ya uchawa? Je, Nyerere alikuwa Chawa na mpumbavu kama Steven? Hapana, Nyerere alikuwa mtu muhimu na mwelewa sana. Sasa, kwann machawa yajiite jina lake? Huo ni udharirishaji wa mtu mkubwa.

Ninaomba watanzania tuepuke hii dhana ya ujinga na upumbavu ya kuwa Chawa na kutumia majina ya watu ili tuwe maarufu. Wakati hiyo sifa hatuna, elimu hatuna.
 
Take it easy bro!don't take it too personal! Steve Nyerere still hana baya,nataka nikukumbushe aka jina la utani linamfuata mtu automatically, na unaweza tumia.gharama kubwa ili uitwe flani na bado jina likakukataa vile vile!! Hivi unajua kua Nyerere alikua halipendi jina la Mchonga lakini bado jina likamfuata kila anapokwenda!? Au kwenye utawala wa Nyerere ulikua bado hujazaliwa!!? Labda useme Steve Nyerere katumia hilo jina kufungua mirathi ya Mwalimu kama na yeye mrithi hapo ndiyo kutakua na kosa kisheria, na ana staili kukamatwa na kuithibitishia Mahakama kua na yeye ni mrithi!!
 
Nyerere ni jina kama yalivyo majina mengine, huwezi kumpangia mtu jina ati kwakuwa linafanana na la kwako.
Jina hilo halijasajiliwa popote ili lisitumike na wengine.
Kuna majina makubwa yanatumika duniani kuliko hilo.
Majina kama Gabriel (jibril)
Jesus (Yesu), Mungu nk.
Kwanini iwe Nyerere!!
Kwa mila za Kizanaki hata Julius Nyerere mwenyewe jina la Nyerere si lake.

Sasa mtu anaanzaje kujipa copyright kwenye jina?
 
Uwezo wa mtoa mada hapo juu hakika ni mdogo sana. Na inadhihirisha kuwa mtoa mada ni mbumbumbu na hana uelewa au ni mzito kuelewana mada.Au ni chawa kama machawa wengine.

Alichoongea Madaraka ni kuonyesha , kuwa kwa kuwa Nyerere alikuwa mtu muhimu na mwenye uwezo mkubwa sana. Basi jina lake lisitumiwe hovyo na watu ambao hawana sifa kama yeye. Mfano Steven hana sifa yeyote ya kisiasa au ya kusimama na kama mwanafarisafa kupambana na kutoa hoja nzito nzito duniani kama Nyerere.

Kwann anaitwa Nyerere. Wakati ana sifa ya uchawa? Je, Nyerere alikuwa Chawa na mpumbavu kama Steven? Hapana, Nyerere alikuwa mtu muhimu na mwelewa sana. Sasa, kwann machawa yajiite jina lake? Huo ni udharirishaji wa mtu mkubwa.

Ninaomba watanzania tuepuke hii dhana ya ujinga na upumbavu ya kuwa Chawa na kutumia majina ya watu ili tuwe maarufu. Wakati hiyo sifa hatuna, elimu hatuna.
Kwa hiyo Steven akiwa chawa anayetumia jina la Nyerere ndiyo tutashindwa kujua huyu chawa?

Huyo Nyerere si mnamuita Baba wa Taifa? Sasa kama kajenga taifa la machawa wananchi wakijiita jina lake kichawa huoni poetic justice hapo?

Julius Nyerere hana copyright ya jina hilo.

Kenya kuna comedian anaitwa Churchill. Winston Churchill alikuwa Waziri Mkuu maarufu kabisa wa Uingereza. Lakini hutasikia Waingereza wanamshobokea comedy wa Kwnya kwa sababu katumia jina la Churchill.

Ni ujinga mtupu.

Sasa mtaanza juweka daftari la watu wote wanaoitwa Nyerere?

Mkimkuta Mmarekani mweusi kaamua kujiita Nyerere mtamfanya nini?

Hao watoto na wajukuu wa Nyerere vichaa wanasema ovyo kila siku kina Andrew, kina Wade etc, nao mtawafanya nini? Mtawaondolea hilo jina la Nyerere?

Madaraka tangu agombanie jina la Nyerere kumuambia mtalaka wake Leticia aache kulitumia alijionesha yuko petty.

Julius Nyerere ni mtu aliyeamini katika usawa wa watu, sasa kwa nini Madaraka anataka kuvunja kanuni hii na kulifanya jina la Nyerere kama jina takatifu linalotakiwa kutumiwa kwa kibaki maalum kama vile si la mtu tu kama watu wengine?

Kwa nini Madaraka anataka kuvunja falsafa alizoziishi Julius Nyerere?
 
Take it easy bro!don't take it too personal! Steve Nyerere still hana baya,nataka nikukumbushe aka jina la utani linamfuata mtu automatically, na unaweza tumia.gharama kubwa ili uitwe flani na bado jina likakukataa vile vile!! Hivi unajua kua Nyerere alikua halipendi jina la Mchonga lakini bado jina likamfuata kila anapokwenda!? Au kwenye utawala wa Nyerere ulikua bado hujazaliwa!!? Labda useme Steve Nyerere katumia hilo jina kufungua mirathi ya Mwalimu kama na yeye mrithi hapo ndiyo kutakua na kosa kisheria, na ana staili kukamatwa na kuithibitishia Mahakama kua na yeye ni mrithi!!
Nani alikwambia kuwa Nyerere hakulipenda jina la mchonga? Aliitwa Mchonga kwa kuwa alionekana kuchonga meno. Na wazanaki wengi wamechonga meno.Kwa hiyo hilo alikuwa jina la mtu mwingine.

Tuwaite majina watu kama wana sifa sahihi, za watu wanaohusika. Tusiwaite majina watu ambao hawana kabisa sifa za hao watu. Huo ni udharirishaji.
 
Madaraka anatetea baba yake na wewe mleta mada tetea baba yako
 
Madaraka alisema hata wao wana mtu anaitwa Steve Nyerere, hivyo inawachanyangaya kujua ni yupi hasa kutokana na matukio mbalimbali.
 
Nimeshangaa sana kusikia huyu jamaa akilia wivu kwa watu wanaomuenzi JK Nyerere kwa namna zao.

Madaraka, mbona sikusikii ukihitaji falsafa zake zilindwe? Kuna taasisi ya Mwalimu Nyerere, Butiku ameigeuza kikao cha ukoo cha wazanaki, anakula hela za Urusi, China, Skandnavia.

Mwalimu alikuwa analina mashamba hapo Butiama, hatujakuona shambani. Kazi kupiga mizinga kwa viongozi.

Enzi za Mwalimu elimu bure, wewe ukaishia kwenye pombe na kulala Magomeni eti unapromote ngumi.

Nyerere ni mkubwa kuliko jina
Jina ndio kila kitu,fikiria gharama ya kuilinda brand,sio kama chama mboga mboga kwao jina brand sii chochote sii lolote mnasema ninyi mnayo mbeleko na zaidi mnazo chawa na kunguni.
 
Madaraka anatetea baba yake na wewe mleta mada tetea baba yako
Huyo Madaraka wenu angekua Prince Charles sijui hali ingekuwaje!!?? Naona ange kamata ma wanawake wote wanaojita Elizabeth jina la Mama yake Queen Elizabeth!! Tena naona ange aanza na Elizabeth Michael a k a Lulu wa Kanumba!!
 
Madaraka alisema hata wao wana mtu anaitwa Steve Nyerere, hivyo inawachanyangaya kujua ni yupi hasa kutokana na matukio mbalimbali.
Hii sababu haina mashiko.

Kwani watu wangapi wana majina sawa?

Mbona hata katika ukoo mmoja unaweza kukuta majina yamejirudia mpaka kukawa na mdogo na mkubwa?

Kwani hakuna middle names? Mbona baba yao Julius tunamjua Julius Kambarage Nyerere, na akija julius Nyerere mwingine ambaye si Kambarage tutamjua huyu tofauti?

Mbona Madaraka kaka yake anaitwa Andrew Nyerere halafu Kenya kuna professor anaitwa Dr. Andrew K. Nyerere?

Na huyo naye wamemuambia aache kutumia jina la Nyerere?

Wanajua baba zao wote wamezaa watoto wangapi?
 
Back
Top Bottom